BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Afisa Polisi Jamii kutoka Mkoa wa Kipolisi Ilala Eugene Mwampondele amesema Kesi 949 kati ya 1,271 zilizopelekwa Madawati ya Jinsia katika Mahakama ya Wilaya mwaka 2018/21 zimeondolewa.
Ametolea mfano takwimu za matukio ya Ukatili wa Kijinsia katika Kituo cha Stakishari pekee yameongezeka hadi 366 kwa mwaka lakini kesi zake hufutwa kutokana na ndugu wa waathirika kuacha kuzifuatilia.
Amesema changamoto kubwa katika kukabiliana na matukio hayo ni kutokuwepo sheria inayomlinda muhanga kupata ufadhili wa matibabu na badala yake analipishwa fedha kama wagonjwa wengine.
======================
Zaidi ya robo tatu ya kesi za ukatili wa jinsia zinazofika mahakamani wilayani Ilala huondolewa, kutokana na ndugu wa wahanga kukacha kuzifuatilia.
Katika jumla ya kesi 1,271 zilizopelekwa na madawati ya jinsia katika mahakama ya wilaya hiyo kwa kipindi cha mwaka 2018/21 ni 949 zimeondolewa.
Akizungumza na Mwananchi digital kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Ofisa Polisi Jamii wa wilaya hiyo, Eugene Mwampondele amesema hiyo ni moja ya changamoto kubwa zinazokwamisha kukabili ukatili wa jinsia.
"Tunafanya upelelezi, tunakamilisha tunapeleka faili mahakamani lakini ndugu wa mwathirika wanachama kufuatilia kwa hiyo moja kwa moja unakuta kesi inaondolewa," amesema.
Ameeleza utaratibu wa mahakama iwapo kesi itapelekwa bila kufuatiliwa mara kadhaa inaondolewa.
Akitoa takwimu za matukio ya ukatili yanayoripotiwa katika Kituo cha Stakishari pekee amesema ni manne hadi matano kwa siku, 30 hadi 40 kwa mwezi na 366 kwa mwaka.
Hata hivyo, amesema idadi hiyo ya matukio yanayoripotiwa ni mara tatu zaidi ya yaliyokuwa yakiripotiwa kabla ya kuanzishwa kwa dawati la jinsia.
Alipotembelea dawati la jinsia la Kituo cha Polisi Stakishari, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wanawake (UN-Women), Sima Bahous amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Polisi kukabiliana na vitendo hivyo.
"Nalihimiza Jeshi la Polisi kupunguza changamoto kwa waathirika wanaoripoti matukio ya ukatili. Hii ni pamoja na kuwajali, kuondoa uzembe, ufisadi, dharau na kutoamini," amesema.
Changamoto nyingine katika kukabiliana na matukio hayo iliyotakwa na Polisi ni kukosekana sheria inayoruhusu muhanga kupata ufadhili wa matibabu na badala yake wanalipishwa hela kama wagonjwa wengine.
"Hii inafanya muhanga hata akiathirika kwa namna gani, atalazimika kulipa ndiyo apatiwe matibabu," amesema Mwampondele.
MWANANCHI