Polisi Njombe Wafafanua Tukio la Kijana Kushambuliwa kwa Tuhuma za Wizi wa Parachichi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Polisi Mkoa wa Njombe imetoa ufafanuzi kuhusu picha mjongeo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha kijana mmoja aliefahamika kwa jina la Ackrey Philipo Ngole(26) Mkazi wa mtaa wa Maheve akishambuliwa na kundi la watu kwa fimbo na magongo Agosti tisa mwaka huu, akihusishwa kuiba matunda ya parachichi.

Jeshi la Polisi mkoani Njombe limesema katika hatua za awali za uchunguzi limewakamata watu wanne akiwemo kijana aliyepigwa kwa tuhuma za wizi wa parachichi na wengine watatu wanashikiliwa kwa kosa la kumpiga kijana huyo na kusababishia majeraha.

Kuhusu hali ya kijana aliyekuwa akipigwa, jeshi hilo limesema hali yake inaendelea kuimarika baada ya kukimbizwa hospitali na kutoa onyo kwa watu kutoendelea kujichukulia hatua mkononi pindi wanapokamata mtuhumiwa yeyote wa wizi.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…