Polisi Tanga waeleza sababu ya kuendelea kumshikilia Bondia Hassan Mwakinyo

Polisi Tanga waeleza sababu ya kuendelea kumshikilia Bondia Hassan Mwakinyo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa sababu ya kuendelea kumshikilia bondia maarufu nchini Hassan Mwakinyo (29), anaetuhumiwa kumshambulia mkazi wa jijini Tanga Mussa Ally akimtuhumu kuwa ni mwizi.

1741614993227.png
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu Machi 10,2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema Mwakinyo anatuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi Mussa Ally ambae anadai ni mvuvi alipopita kwenye makazi yake.

1741614907785.png
Kamanda huyo amesema uchunguzi utakapokamilika atatoa taarifa kwa vyombo vya habari ikiwa ni sambamba na kumfikisha mahakamani ili ajibu tuhuma zitakazomkabili.

Amesema wamemkamata kwa tuhuma za kumjeruhi mvuvi, ambapo ni tuhuma za jinai mtu yeyote akifanya makosa kama hayo bila kuangalia nafasi yake kwenye jamii, anatakuwa kuchukuliwa hatua za kisheria na suala la umaarufu haliwezi kubadili kile kilichotendeka.

"Jeshi la polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia Hassan Mwakinyo (29) mkazi wa Sahare jijini Tanga kwa kumshambulia na kumjeruhi Mussa Ally mkazi wa eneo hilo ambae ni mvuvi,uchunguzi wa tukio hili unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atapelekwa mahakamani," amesema Mchunguzi.

Soma, Pia
 
Naomba uchunguzi uchukue mwaka mzima ili kuwa na uhakika
 
Kamanda mwenyewe kijana kabisa lakini mabegani mfachu yaani kachafuka mabegani ile mbaya
 
Back
Top Bottom