Mukuru
Member
- Apr 14, 2009
- 40
- 0
JESHI la Polisi limepokea msaada wa simu 100 kwa ajili ya kuwasaidia polisi waliopo wilaya za Tarime na Rorya, mkoani Mara kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika maeneo ya mapigano yanayotokea mkoani humo. Msaada huo wa simu ulitolewa jana na mfanyabiashara wa simu za mkononi, Zahoro Khamisi, maarufu kama Matelefone kama mchango wake kwa polisi jamii.
Akikabidhiwa msaada huo katika makao makuu ya Polisi, Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kwa niaba ya jeshi hilo, alisema Matelefoni amekuwa mdau muhimu katika kulisaidia Jeshi la Polisi na matukio mbalimbali ya kijamii.
Alisema mwaka huu katika kipindi cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), Matelefoni alitoa simu 350 kwa ajili ya mawasiliano kwa walemavu hao, ili kurahisisha kutoa taarifa pindi wanapomuona na kumjua mhalifu.
"Kwa kuwa aliguswa na mauaji hayo na jana alitoa simu 100 zenye thamani ya sh milioni 4.5 kwa ajili ya kuwasaidia polisi waliopo Tarime na Rorya kutekeleza majukumu yao ipasavyo," alisema Kova.
...................................................................................................
😕...Najua misaada ni mizuri ila nakuwa na wasi wasi vyombo vya serikali vinapopatiwa "misaada" na watu binafsi ikiwemo wafanya biashara. Ninadhani hii inaweza kuathiri utendaji wao kwa kuwafumbia macho hao 'watoa misaada'...ni mtazamo wangu. WanaJF, nyie mwaonaje?