Polisi: Tunachunguza kifo cha mtu ambaye mwili wake ulikutwa unaelea mto Msimbazi

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
03 Mei, 2026

TAARIFA KWA UMMA
​
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linachunguza kifo cha mtu ambaye tarehe 30 Aprili, 2026 saa 09:00 Alasiri mwili wake ulikutwa unaelea kwenye maji yaliyokuwa yanatiririka katika mto Msimbazi eneo la Kipawa Wilaya ya Ilala. Mwili huo ambao haukuonekana kuwa na kichwa baadae uchunguzi wa awali umeonesha unaweza kuwa wa mtu aitwaye James Temba mkazi wa Tabata Chang'ombe Wilaya ya Ilala.

Uchunguzi wa tukio hili unaendelea ili kubaini chanzo cha kifo hicho na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuhusika.

Imetolewa na;

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam



Pia soma Mwili wa James Temba, aliyepotea umeokotwa mto Msimbazi ukiwa hauna kichwa
 
Hv kwamba n akili ndogo kujua kutupa mwili kwenye utaonekana tuu au?
 
Kuna kesi zenye ushahidi km mzee kibao mpk leo. Aaah kifo ni kifo tuu ndiyo majibu yao.
 
Vichaa wakubwa hawa, huo uwezo wa kuchunguza wameutoa wapi?. Si ajabu wenyewe ndio wanaohusika au wanajua nani yuko nyuma ya huu mchezo.
 
Ila polisi wetu dah..ila siku kosa lao, wale vilaza kweli kweli wa sekondari saiz ndo wapelelezi wa makosa ya jinai!
 
Ndiyo imeisha hiyo. Hilo jeshi halina credibility yoyote ile kwa wananchi.
 
Hawa polisi wanafikiri kwa kutumia makalio na mikwundwu. Inakuwaje watoe taarifa ya kipuuzi kama hii wakati mauaji ya James yanajulikana wazi kabisa?
 
Hii siku iliokotwa miili miwili, dah yule mwingine ndiyo ilizimwa kabisa. Swala la uhai wa raia ni kipengele sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…