Polisi Uganda wavamia kituo cha ukusanyaji wa kura kisicho cha Serikali

Polisi Uganda wavamia kituo cha ukusanyaji wa kura kisicho cha Serikali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Polisi nchini Uganda wamevamia hoteli moja ambako kikundi cha wanaharakati wa mashirika ya kiraia na wakaguzi wa uchaguzi walikuwa wamekusanya taarifa kutoka kwa waangalizi wengine wa uchaguzi tofauti na Tume ya uchaguzi.

Msemaji wa polisi nchini humo, Bw Fred Enanga amesema kuwa walipata taarifa za ujasusi kwamba baadhi ya wanaharakati wa kiraia walikua wameweka kituo chao cha ukusanyaji wa matokeo ya kura katika Hoteli Africana iliyopo mjini Kampala , kando na kituo cha taifa kinachokusanya matokeo ya uchaguzi wa rais na wabunge.

“ Tulituma watu wetu katika Hoteli Africana. Watu wenye jukumu la kudhibiti uchaguzi ni Tume ya uchaguzi. Huwezi kujua ni nini kilicho nyuma ya kituo hiki cha ukusanyaji wa matokeo ya kura. Huenda wana nia mbaya ambayo inaweza kuchochea ghasia . Sheria inaruhusu Tume ya uchaguzi tu kutangaza mataokeo. Kuwa na kituo cha kukusanya matokeo kando kunashusha hadhi ya uchaguzi na tume ya uchaguzi,” Bw Enanga aliiambia NTV Uganda.
 

Attachments

  • 1610699759800.gif
    1610699759800.gif
    42 bytes · Views: 2
  • Thanks
Reactions: Lee
Mmmh,washachakachua ndio maana hawataki watu wengine wakusanye matokeo kutoka vituoni!
Nchi za Africa sijui nani aliziloga!
 
Hakuna Chaguzi wala demokrasia duniani, mwenye nguvu ndie mtawala
 
Back
Top Bottom