Parable
Senior Member
- May 2, 2012
- 192
- 153
kama RAIA halali wa nchi hii name wengineo tutakubaliana kuwa jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kulinda RAIA na mali zao..sasa hilo jukumu jana nimeona 'likigeuzwa kichwa chini miguu juu'
kijana mmoja (jina limehifadhiwa) alikuwa akipiga debe stendi ya moshi, baada ya muda ikaja gari ndogo aina ya corrola ikiwa na watu wanne ndani yake. Kwa kudhani wale ni abiria kijana akawakaribia akiwajulisha uwepo wa basi la muda huo na mengineyo ambayo walipaswa kujua.
Wale watu wakasema hawana safari, hivyo basi kijana akaendelea kutafuta abiria wengine kama njia yake ya kila siku kujipatia kipato
kumbe abiria wale walikuwa askari na baada ya muda wakamsuspect kwa tukio la wizi wa simu..wakamchukua kinguvu kwenye gari yao wakisema anapelekwa central police kumbe wakampeleka sehemu tofauti na kumpiga sana kwa vyuma vilivyokuwa ndani ya hiyo gari na baadae kumwachia huru.
Nilimpa ushauri pia nikaenda naye kituo cha karibu cha polisi name kuripoti uvunjaji huo wa haki ya kimsingi ya binadamu pia nikahakikisha anatibiwa kwenye hospitali ya serikali maana hakuwa na pesa na aliumizwa vibaya sana
Sasa swali ambalo sikupata jibu lake mpaka sasa no kuwa..ikiwa itagundulika kuwa wale ni askari na la mmoja wao lilipatikana pamoja na namba za gari..polisi wanajibu vipi mashtaka hayo ya ukiukwaji wa haki za binadamu?
naomba kuwasilisha