Polisi wa Kenya ni Aibu

nashangaa baadhi ya watz mnavyo onyesha unafiki wa kuwaonea huruma wakenya kwa haya wanayo yapitia.

mimi siwaonei huruma...acha wauwane wao kwa wao.

sababu ya kutowaonea huruma ni ile kauli inayotolewa na baadhi yao kwamba wao ni "aggressive" sana....eti wanapoanzisha movement hawarudi nyuma mpaka wafanikiwe...acha GSU iwanyoroshe... Cc MK254
 
Unajua hao Polisi ni binadamu pia wanajua Raila is a President in waiting! Kila mtu mwenye kutoa maamuzi ana wasiwasi huko...
 
Hivi wewe kwanini hueleweki?, hapa kinachozungumzwa ni Kenya, wewe unarudisha Tanzania, nani aliyekuambia kwamba kwasababu yanafanyika Tanzania kwahiyo ni halali kufanyika Kenya?, hapa Tanzania tuambia ni watu wangapi waliouliwa wakati wakiandamana?, watu wanazungumzia kinachoendelea Kenya, wanalaani mauaji yanayofanya na polisi huko Kenya, wewe unataka wakae kimya ili huku nako watu wakiuliwa wakenya wasilaani nao wakae kimya?
 
Naeleweka sana, ninachosema ni kuwa yanayotokea Kenya yamewahi na yanatokea EAC yote!! Kwetu hapa mauaji yametokea mengi na makubwa kuliko hayo ya Kenya eg 2001 Zanzibar!! Nani alilaani?! Si mkenya wala mnyarwanda !!Arusha (ollasiti) nani amelaani?! Si mrundi wala mganda. Tunafanana sema kidogo wapinzani wa Tz busara ya kujizuia ipo!! Ukuta 2016 wasingejizuia mauaji yangalikuwa makubwa zaidi. Wenzetu huko hawajizuii

Africa hasa Africa mashariki ni mbaya zaidi. Watawala kupitia police huwaona wananchi wao kama maadui zao. Kenya imeingia mtego huo. Katika siasa bora kidogo sasa Africa magharibi, watawala wanapata shinikizo la kukubali maamuzi ya wananchi .
 
Hivi umeona support aliyonayo? MTU kama Yule huwezi deal nae kijinga.
It will cost a nation, like 2007. Usimlinganishe Odinga na wapinzani uchwara wengineo EA.
 
Arafu huyo mpumbaavu wa jeshi la polisi bado anapokea mshahara na makamanda wenzake wakati jeshi ni bovu wameshindwa kuliongoza hata hapa tz kuna uchunguzi ulionyesha polisi na mahakama ndiyo zinaongoza Kwa rushwa lakini cha kushangaza bado makamanda feki walioshindwa kazi na wausika wa mahakama wanaendelea kulipwa mishahara bure huu ni uhanithi wa AKILI arafu utasikia watu wanalaumiwa kwa kujichukulia sheria mikononi stupid manki
 
Hivi umeona support aliyonayo? MTU kama Yule huwezi deal nae kijinga.
It will cost a nation, like 2007. Usimlinganishe Odinga na wapinzani uchwara wengineo EA.
Kwa hiyo sababu anajua ana support ya watu wengi ni iwe kigezo cha kuleta machafuko...kisa uongozi....kwa nn asitumie huo umashuhuri wake positively ili watu wasipoteze maisha bila sababu za msingi...sisi miafrika sijui tunanatatizo gani tu...??Huku wakina Kagame wanaua wapinzani, ukienda Zimbabwe hakueleweki, Tz chokochoko zimeanza za ajabuajabu, Burundi ndo shida tu, Sudan ya Kusini ndo vita vya nje nje....Kenya ndo akili zote Odinga anacontrol...HAKUNA mtu wa kushauri mwenzake..East Africa inawakati mgumu sana
 
chadema wenzangu wanao sapoti serikali ya uhuru njooni hapa tu comment ushabiki

At the same time waandamanaji wanachoma maduka na kupora vitu, iyo ni ghasia. Haifanani na maandamano yanayofanyikaga hapa nchini. Hao watu wa raila sio wadai haki, ni wafanya fujo. Do you know how to deal with them? Any suggestions?
 
Mauaji yote yanayotokea watu wote wanalaani, mauaji ya Zanzibar yalipotokea, dunia nzima ilipiga kelele kama utakumbuka hadi ikaundwa tume ya jumuia ya madola kuja kusuluisha na Zanzibar iliwekewa vikwazo na jumuiya za kimataifa, au kulaani unakotaka wewe ni kupi?, idadi hadi sasa inayojulikana waliokufa Zanzibar ni 27 kulingana na serikali na 32 kulingana na jumuia za kimataifa, ndiyo mauaji makubwa kati historia ya Tanzania kutokea kwa pamoja, Kenya katika kipindi hiki pekee tangu August hadi sasa kabla ya jana ni watu 37, ukiongeza hawa watano wa jana ni 42, hiyo ni mbali na wale waliokufa 2007 ambao ni zaidi ya 1200, sasa wewe unaposema Tanzania mauaji ni zaidi ya Kenya unatoa wapi hizo data zako zaidi ya kutaka kuzungumzia ushabiki na udaku?

Kwani huko nyuma maandamano yalikuwa hayafanyiki, mbona watu hawakuuliwa kama wanavyouliwa Kenya?, kama ni kuzuiliwa kwa maandamano ni kipindi hiki cha Magufuli, kwanini unataka kuonyesha kwamba polisi wetu ni wakora zaidi ya Kenya, wakati wa vipindi vilivyopita kumekuwa na maandamano lakini yalitawanywa kwa mabomu na maji ya kuwasha pekee?, ripoti za dunia nzima zimeiweka polisi wa Kenya kuwa ni namba 3 kwa mauaji ya kiholela, na inaongoza Afrika kwa kuua watu kiholela, wewe hizi data za kusema Tanzania hali ni mbaya zaidi ya Kenya umezitoa wapi, tunaomba vyanzo vyako, kinyume cha hapo, hayo yatakuwa ni maneno yako yasiyo na ukweli wowote.
 
Tumelaaniwa.....au ni logo au kitu gani sijui.
 
chadema wenzangu wanao sapoti serikali ya uhuru njooni hapa tu comment ushabiki
Bado huwezi kuifananisha Kenya na nchi wanachama wenzake wa Afrika Mashariki..

Na kumbuka pia mtu kuiunga mkono serikali ya Kenyatta sio kwamba wanaunga mkono kila kitu kama walivyo watu wa chama kimoja hapo wakiunga mkono wanaungana hadi kwenÿe maovu.

Uhuru ameonesha kujiamini vya kutosha na hiyo ndio tabia ya mwanaume..

Kuna nchi hadi vilema wakiandamana wanapigwa kama wezi waliotua mikononi mwa raia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…