Polisi wa kumwaga wapelekwa kilindi

Polisi wa kumwaga wapelekwa kilindi

dionsio

Senior Member
Joined
Oct 11, 2013
Posts
169
Reaction score
29
Idadi kubwa ya askari polisi FFU imepelekwa wilayani kilindi ili kuongeza nguvu kwa askali wenzao ambao inaonekana kuzidiwa nguvu na kundi lililofanya vurugu iliyosababisha kujeruhiwa kwa risasi OCD wa Kilindi.

Kundi hilo liliwasili hapa handeni majira ya saa 5 usiku, likitokea kibaha pwani, na lilikua linaongozwa na mkuu wa wilaya ya kibaha. Msafara huo ulipita kuonana na mkuu wa wilaya ya handeni ili kupata maelekezo toka kwa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa tanga, ambao walikutana hapa handeni kujadili hali tete ya handeni.

Kikao hicho kilidumu takribani masaa 5 tangia saa 9 hadi 1 ucku. Kikao hicho kilifanyika HILL TOWN HOTEL.
 
Kila la heri kwenye"Wapigwe tu,Maana Tumechoka"
 
Ikiwa serikali ingesoma taarifa mbalimbali toka hapa JF wala hakungekuwa na hiyo tabia ya zimamoto ya ulinzi. Mnapoambiwa ndani ya misikiti kuna mazoezi yasiyoendana na mila za dini zetu na kwamba nchi imeingiliwa na chembe za magaidi mnatufanya ni wachochezi. Tumetoa pendekezo la kuimarishwa kwa mabalozi nyumba kumi serikali yetu inajifanya haisomi hapa JF. Hakika wangesoma ujumbe unaoihusu Chadema hapa JF wangefuatilia hadi mwisho wake.
 
Wanataka kuwafurahisha baadhi ya watu. Zilitolewa mpaka CD bungeni zilizorekodiwa watu wakilishwa sumu ya Udini, UDOM, wahusika walialikwa na akina Nkamia, maCCM, mapovu yakawatoka kupinga, kisa ameileta mpinzani. Yanayotokea leo ni matunda ya kupuuzia taarifa nyingi wanazopewa. Pale Mwananyamala, kuna msikiti watu wanajifunza karate, jirani yake kuna kanisa watu wanajifunza ufundi cherehani, Useremala na computer. Baadae kuna kundi litaibuka na kudai kwamba linanyimwa ajira!
 
hiyo ndiyo hali halisi. Madhara ya kutawaliwa na wababaishaji.
 
Bubu Msemaovyo umesomeka vema katika post yako.
Wangekuwa wanapitia hapa kupata yote yanayoendelea hakika wangekuwa mbali sana.

Ila nina Imani ya kwamba sasa imesalia muda mchache wawe wanapapitia.

Kila la kheri mapolisi!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom