Leo mida ya saa kumi nimeenda kibaha kwa mathias. Nikiwa narudi maeneo ya kibaha stand nikasimamishwa na trafiki. Wakasema kosa langu niliovertake maeneo ya miembe saba nikasimamishwa nikakimbia. Nikamwambia nitakuwa sio mie labda mtu mwingine kwa kuwa mie nimeishia kwa mathias na miembe saba ni mbele zaidi ya hapo ambako sikufika...yule polisi akasema basi mngoje alietoa order ukamatwe. Nikakaa hapo kibaha kituoni kwa zaidi ya saa moja uku wadada mapolisi wakinidhihaki kwa maneno ya taarab.baadae akaja huyo alieniona na sura yake ikilazimisha rushwa akinitishia kunipeleka mahakamani.Bahati nzuri akatokea askali mmoja akiitwa Mikidadi akamsihi sana huyo afande aniachie. Ndipo akaniachia kwa shingo upande baada ya kuwa kanisumbua kwa masaa mawili bila kosa....nikasema hawa ndio polisi wa Tanzani wenye kiu ya rushwa kwa kiwango cha kusingizia watu makosa. Naamini siku moja Watanzania watasema NO enough is enough.