Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limeanza kufuatilia taarifa ya kupotea kwa Daisle Simon Ulomi, mfanyabiashara ambaye hakurudi nyumbani kwake toka alipoingia kazini kwake siku ya tarehe 11 Desemba, 2024 baada ya taarifa ya kutafutwa kupokelewa katika kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke mnamo Desemba 12, 2024.
Taarifa ya leo Desemba 14, 2024 iliyotolewa na Kamanda Kanda Maalum ya Polisi, Dar es Salaam SACP Muliro J Muliro imeeleza kuwa siku hiyo Mfanyabiashara huyo alionekana akitoka Ofisini kwake Sinza Kijiweni majira ya saa 6:00 mchana kuelekea Mbagala, Bandari kavu alikodai anaenda kukagua ‘container’ la bidhaa zake baada yakuitwa na watu aliodai ndiyo waliokuwa wanashughulika na kutoa kontena hilo bandarini na alikuwa akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe.
Jeshi la Polisi limesema linafuatilia taarifa hiyo kwa kushirikiana na ndugu ili kujua na kubaini mtu huyo yupo wapi huku likitoa wito kwa yeyote mwenye taarifa kuhusiana na mtu huyo azitoe kwenye mamlaka yoyote ya Serikali iliyo karibu yake.