Polisi waanza kutekeleza agizo la Gambo

Polisi waanza kutekeleza agizo la Gambo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limeanza kuyafanyia kazi maelekezo ya mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyeagiza watu wanaosambaza mitandaoni video za ubovu wa barabara za kwenye hifadhi kukamatwa




Polisi imemtaka Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kutoingilia suala hilo. Mrisho Gambo aliagiza Polisi kuwasaka, kuwakamata na kuwahoji waliotumia Mitandao ya Kijamii kuonesha ubovu wa miundombinu ya barabara ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Gambo alisema watu hao wanachafua taswira ya nchi na wana lengo baya kwani kulikuwa na njia sahihi kuliko kutumia mitandao ya kijamii; kitendo alichokifananisha na Uhujumu Uchumi

Pia soma:
Uhujumu Uchumi: RC Arusha ataka waliosambaza video ikionyesha barabara mbovu mbugani kukamatwa mara moja
 
Hawa viongozi wetu wamevuta bangi ya wap?
 
Mwaka huu tutaona mengi sana kama kila kitu ni uhujumu uchumi
 
Piga kazi gambo aibu ya ndani huwa haitolewagi nnje
 
Aanzee kwa kuwakamata hao kwanza kama yeye ni kidume kweli


 
Ana masters kutoka pale chuo cha uhasibu Arusha,ndio elimu yetu hio.
 
Back
Top Bottom