Jeshi la Polisi mkoani Arusha limeanza kuyafanyia kazi maelekezo ya mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyeagiza watu wanaosambaza mitandaoni video za ubovu wa barabara za kwenye hifadhi kukamatwa
Your browser is not able to display this video.
Polisi imemtaka Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema kutoingilia suala hilo. Mrisho Gambo aliagiza Polisi kuwasaka, kuwakamata na kuwahoji waliotumia Mitandao ya Kijamii kuonesha ubovu wa miundombinu ya barabara ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Gambo alisema watu hao wanachafua taswira ya nchi na wana lengo baya kwani kulikuwa na njia sahihi kuliko kutumia mitandao ya kijamii; kitendo alichokifananisha na Uhujumu Uchumi