Polisi wafanya unyama mpya mgodini Nyamongo

Hapa tunazungumzia suala la Nyamongo. Suala la morogoro na iringa hata mimi natupia lawama polisi. Kweli ukweli nasema ukweli

Ulishawahi kujiuliza ni kwanini askari polisi wanagombania kupangiwa kazi kituo cha nyamongo? ushawahi kujiuliza ni kwanini askari polisi wanatoa rushwa kwa wakuu wao ili wapangiwe kituo cha nyamongo? ushawahi kujiuliza ni kwanini askari polisi wanaofanya kazi mgodini nyamongo wana utajiri mkubwa usiofanana kabisa na kipato chao cha upolisi?

Haya mambo mnapoyajadili msiwe kama mbuni, jitahidini kuangalia kwa upana wake. Mkikaa kusikiliza propaganda za ccm na serikali yake ndio mnabaki kuandika vitu vya hovyo hovyo against watu wa Tarime. Na kwa taarifa yako hata kama polisi wataendelea kuua watu kila siku, watu wa nyamongo na tarime kwa ujumla hawatachoka kupigania haki yao hadi hapo itakapopatikana hata kama ni kwa gharama ya uhai wa watu wengi kiasi gani.
 

Mkuu hapa kila mtu anaongea kadri anavyofahamu. Kama nimekosea nyoosha sentensi na wengine wafahamu ukweli kuhusu mgodi wa nyamongo. Usipende kukimbilia matusi siyo mazuri sana
 

Kuna watu hapa jamvini wamerukwa na akili kiasi kwamba wakisikia watu wa nyamongo na tarime wameuwawa na polisi wanajisikia raha mioyoni mwao kiasi wanasahau kwamba watu wa nyamongo nao ni binadamu na wako nchini mwao na wana haki ya kuishi na kufaidi rasilimali walizopewa na mwenyezi Mungu.

Mgodi umetiririsha maji yenye sumu kuingia mto tigite ambao unategemewa na wananchi wote wanaoishi kuzunguka mgodi kwa ajili ya maji ya kutumia wao pamoja na mifugo yao lakini serikali imekaa kimya na hata hawa wapiga porojo hapa nao wamekaa kimya. Lakini wakisikia mtu wa nyamongo kauwawa ama kajeruhiwa kwa risasi ya moto na polisi ndio wanakuwa na kiherehere cha kuwasema vibaya watu wa nyamongo.
 
Hao wananchi walipigwa tu bila sababu za msingi? Kama walivamia eneo la mgodi, sidhani kama kulikuwa na makosa upande wa askari. Askari walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi kama kawaida.

Tuendelee kuishi tu huku tulikojilipua au kuletwa na ndugu zetu kwa kufanyiwa mipango; na kushiriki katika mijdala inayohusu nchi yetu kupitia keypad !!!
 
Hao wananchi walipigwa tu bila sababu za msingi? Kama walivamia eneo la mgodi, sidhani kama kulikuwa na makosa upande wa askari. Askari walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi kama kawaida.

This is ridiculous!Hivi wajibu wa askari wa Tanzania ni kuua?
 

Mkuu Mwita Maranya, hayo yote nakubaliana na wewe. Tunachojadili leo ni issue iliyoletwa na mwenzetu kiribo kuwa polisi wamevamia barabara na kuanza kupiga wananchi. Tunachojiuliza ni nini kimesababisha polisi wakafanya hivyo. Mimi sababu iliyopelekea polisi kutumia nguvu, nimeisema na wewe sema yako. Usiwe na dhana kwamba wewe pekee ndo unajua mengi kuhusu nyamongo. Hayo ni madogo, tunafahamu makubwa zaidi ya hayo ya polisi. Mind your tongue
 
Last edited by a moderator:
This is ridiculous!Hivi wajibu wa askari wa Tanzania ni kuua?

Siyo askari wa Tanzania tu. Dunia nzima kazi ya askari ni kulinda usalama wa raia na kuhakikisha amani inadumishwa katika jamii. Theoretically, utatarajia kuwa matumizi ya nguvu za aina yoyote ile huwa hayahitajiki kufanywa na polisi muda wowote ule. Hata hivyo pale ambapo usalama wa raia unahatarishwa na raia wengine, polisi huwa 'wanalazimika' kutumia nguvu ili kuokoa hawa waliopo hatarini. Logic hapa ni kwamba ni afadhali kuua watu wachache kwa maslahi ya usalama ya watu wengine.
 
This is ridiculous!Hivi wajibu wa askari wa Tanzania ni kuua?

Hivi watu wengine huwa mnafikiri mnachokiandika au mnapumua tu. Hapa tunaongelea polisi kupiga wala siyo kuua. Ndo tunajiuliza wamepigwa bila sababu?
 

Siyo kweli. Wajibu wa polisi ni kulinda raia na mali zao. Polisi anapaswa kutumia njia mbalimbali za kukabiliana na raia. Ndiyo maana kuna mabomu ya machozi, maji ya kuwasha, risasi za mpira. Pia wana vifaa na zana madhubuti kujikinga na mawe n.k. Lakini pia mafunzo ya polisi yanamwezesha kupambana na raia kwa kutumia mikono ana miguu yake wakisaidiwa na mbwa au farasi. Polisi wetu ni wavivu ila mafunzo wanayo hivyo wanapenda short cut
 

Is that logic, works on Iringa "Mwangosi saga", Morogoro - muuza gazeti saga, au sijakupata vzr, au hata hio issue ya nyamogo iko sawa tu, ni kwa masilahi ya wegi akina nani? wewe na mimi tupo kwa hao wengi?Nitakuwa ok kama utasema kuwa "polisi wanafanya hivi kwa ajili ya kupiga mkwara kwamba na wewe ukifanya hivi tutakuua!ambao pia kwangu mimi bado ni upumbavu ule ule
 
Mwita Maranya ninachosema ni kwamba hali ya usalama maeneo ya Nyangoto, Kewancha, Nyabigena si nzuri hata kidogo. Najua unafahamu kwamba wakurya wana silaha za moto na huwa wanaenda kwenye migodi wakiwa kamili na polisi huwa wanatymia risasi kupiga juu kuwatawanya. Hiyo hali kwa Nyamongo ni ya kawaida sana na Polisi pia hupigwa hata ukiona magari ya Polisi yaliyopo kule Nyammongo utajua tu kule ni kama kuna vita. Suala hapa si Polisi kuua ama Polisi kuuawa, suala la msingi ni kutafuta suluhu kati ya Wanyamongo na wawekezaji kwa kuwa Wanyamongo siyo kwamba wanawachukia Polisi bali wanyamongo wanapigania haki yao. Hapa kuna uchonganishi kati ya Polisi na Wanyamongo na mwisho wa siku ni sisi Watanzania kuuana wakati wazungu wanakunywa kahawa makwao. Hakuna pumba. Sitegemei nawe kutumia neno hili mfu.
 
Last edited by a moderator:


Je askari wetu wanaweledi wa hayo unasema hapo? angalia kwenye thread hapo: unaambiwa tarehe 29 watu 3 wameuwawa!
 
Wananchi huwa wanavamia kwenea kutafuta mabaki ya madini wakiwa katika makundi na silaha za jadi.

Mkuu Kimbunga akili ya kuambiwa changanya na zako.
Kwa taarifa yako wakurya ni kawaida yao kutembea na silaha za jadi kama vile sime, panga, jambia, rungu ama silaha nyingine yoyote ya jadi wakati wowote hasa huko vijijini. Kwahiyo usijaribu kujustfy uongo wako hapa kwa kitu ambacho hukifahamu vizuri.

Mnapokwenda huko nyamongo ama Tarime ni vizuri muende mkiwa na akili ya kutaka kuujua ukweli kuliko mnavyokwenda na propaganda mlizolishwa na serikali yenu halafu mnakwenda kutafuata justification ya hizo propaganda kwa kubase kwenye hoja na ushahidi dhaifu kama huu wa kwako.
 
Last edited by a moderator:

Acha kudanganya umma wa watanzania wewe. Yaani polisi wavamiwe na watu wenye silaha kali halafu eti wao wajikinge kwa mikono na miguu na risasi za mpira? Hayo mafunzo gani ya hali ya juu waliyoyapata ambayo yanawawezesha kupambana hadi na mabomu. Wewe inaelekea huelewi hali halisi ya Nyamongo ndiyo maana hujui kwanini vifo vinatokea kule.
 

Mkuu Mwita Maranya linapofika suala la Nyamongo na Wakurya huwa sipendi saaaana kuingia katika malumbano kwa sababu ambazo nazijua na kuna siku nitakupa hizo sababu. Wakurya ni kweli huwa wanatembea na sime lakini siyo kama wamasai.
 
Last edited by a moderator:

Sasa Polisi kama unafahamu makubwa inakuwaje haya madogo unashindwa kuyaelewa? ikiwa serikali imewapa kibali polisi wa nyamongo kuua raia wakati wowote wanapojisikia unatafuta ushahidi gani au sababu gani? ni juzi tu tarehe 29 August wameuwawa watu watatu na polisi na maelezo ni hayo hayo ya kila siku kwamba walikuwa wanataka kuvamia mgodi. Imefika mahali sasahivi polisi wa nyamongo wanawachukulia wananchi thamani yao ni sawa na kuku ambaye anytime t ukiamua kumchinja unachin ja tu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwita Maranya linapofika suala la Nyamongo na Wakurya huwa sipendi saaaana kuingia katika malumbano kwa sababu ambazo nazijua na kuna siku nitakupa hizo sababu. Wakurya ni kweli huwa wanatembea na sime lakini siyo kama wamasai.
Kimbunga kama ungekuwa umenisoma kwa umakini ungegundua kwamba nimesema wakurya wanatembea na silaha za jadi wakati wote wanapokuwa huko vijijini na sikuwafananisha na wamasai.
Toafauti ya wakurya na wamasai ni kwamba wamasai wao hata wakija mjini wanaendelea kutembea na sime zao, wakati wakurya hawatemnbei na zana hizo wakiwa mijini.
 
Last edited by a moderator:


Mbona kwenye matukio ya uhalifu majambazi wanapokuwa wanakwiba huwa hatuwaoni hao polisi wakijitokeza kuonyesha uhodari wao wa kukabiliana na majambazi? wakisikia raia wasio na chochote wanaandamana ama kudai haki yao ndipo utawaona matumbo yao kimbelembelle kwa kujifanya wajuzi wa kutumia risasi za moto na mabomu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…