Polisi wafanya unyama mpya mgodini Nyamongo

Nimetoka Nyamongo Jumamosi asubuhi, sina uhakika kwa shambulizi hili la polisi unalolizungumzia lakini Ijumaa jioni wananchi ambao kule wamezoeleka kama Intruders, walivamia mgodi muda wa kama saa kumi na mbili jioni na kuanza kupiga mawe magari na watu wote waliokuwamo mgodini.

Kuna watu wengi tu wanaofanya kazi mgodini wameuawa kwa kuchinjwa au kupigwa mawe na hao intruders. Hivi sasa magari yote kule mgodini inabidi yawekewe wiremesh madirishani kuepuka kupigwa mawe na hao intruders. Kama mmesikia hivi karibuni ABG wanataka kuuza migidi yao hapa nchini na moja wapo ya sababu ni uvamizi kwenye migodi haswa Nyamongo ambao umewatia haswara kubwa , ikiwa ni pamoja na kuamua kujenga ukuta mkubwa kuzunguka mgodo bila mafanikio kwani jamaa wanapanda na kuvamia frequently.

Pamoja na yote hayo mimi sikubaliani kabisa na kitendo cha polisi kupiga raia wasiokuwa na hatia, au kutumia nguvu kubwa kupita kiasi. Lakini kwa hali iliyopo Nyamongo, jamani naomba muulize walioko kule ni hatari sana. Jamaa wanavamia watu mradi tu wakikuona na gari au kuhisi una chochote wanaweza faidika nacho wao wanaona wewe ni halali yao.
 

Mkuu, sehemu zenye maslahi makubwa pia huhitaji ulinzi mkubwa. Migodi ni moja ya sehemu kama hizo ambazo huhitaji usalama wa hali ya juu hasa ukizaingatia mapato yanayotoka hapo. Kwahiyo sidhani kama upo sahihi kulinganisha ulinzi katika sehemu za kawaida na ule wa sehemu ambazo si za kawaida. Kwa vyovyote hatuwezi kuhalalisha mauaji yasiyo na sababu juu ya raia, lakini hatuwezi kuhalalisha vilevile wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuhatarisha maisha ya wengine.
 
Hao wananchi walipigwa tu bila sababu za msingi? Kama walivamia eneo la mgodi, sidhani kama kulikuwa na makosa upande wa askari. Askari walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi kama kawaida.

Nani ka kwambia wajibu wa Polisi ni kuua raia na si kuwalinda?
 
Mkuu, kwani hujawahi kusikia wazee wa kazi wanaenda kupiga tukio kwenye magodauni usiku wakiwa wamesindikizwa na defender za polisi?!!

Kweli mkuu hawa ni wazee wa dili, kama unavyokumbuka ni juzi tu wamekurupushwa wakipiga mzigo wa shaba bandarini.
 

Mkuu, issue hapa ni namna gani jamii inayozunguka rasilimali hiyo ya asili inavyonufaika na uwekezaji huo wa barrick. Mbona maeneo mengine angalabu hakuna matatizo kama yaliyopo nyamongo? Kwa nini barrick hawatoi service charge katika wilaya ya Tarime na badala yake wanatoa mrahaba tu? Kwa nini resolute ya nzega wanatoa service charge? Kumbuka sheria inatambua service charge na si mrahaba. Tatizo la watz ni kudeal na watu badala ya mfumo
 
Last edited by a moderator:
Vipi upo mwezini?unaongea kama juha????au nawe ni gamba?ukimaliza siku zako njoo uchangie mada upya.....umeelewa radhia?
 
Je askari wetu wanaweledi wa hayo unasema hapo? angalia kwenye thread hapo: unaambiwa tarehe 29 watu 3 wameuwawa!

Ndo maana nimesema askari wetu wanapenda short cut
 

Juzi wamechukua milioni mia nne (400m) benki ya cba, hiyo ni pesa ndogo kwa akili yako?
Huo mgodi una mchango gani kwa maendeleo ya nchi na wananchi wa nyamongo/tarime kwa ujumla wake? Hata hivyo hakuna maana kwamba sehemu yenye uwekezaji mkubwa na yenye ulinzi mkubwa ndio askari npolisi wanaruhusiwa kuua raia kiholela.

Hata kama tukikubaliana kwamba wananchi wale ni wakosefu lakini polisi hawajakasimiwa mamlaka ya kutoa hukumu ya kifo dhidi yao. Kama kweli polisi wetu wamefundishwa kama wanavyofundishwa polisi wa nchi nyengine, tungetarajia kuona wahalifu wote (wavamizi wa mgodi) wakikamatwa na kufikishwa mahakamani.
 
Polisi kuna wakati inabidi atumie silaha za moto si kwa kutaka ila pia kujilinda naye ili asiuwawe.Maana wale watu wa Nyamongo hata ukipiga mabomu ya machozi wao wanakuwa na silaha za jadi utamwona bado anakufuata tu na wewe kama askari ili unusuru uhai wako inabidi utumie risasi za moto ili kujilinda.Utumiaji wa silaha za moto unakuwa mbaya tu pale askari anapolenga/anapozitumia kwa mtu ambaye hana silaha kwa ajili ya kumdhuru askari.
 

Unatia chumvi ili ikusaidie nini?
Barrick wametangaza kuufunga mgodi wa tulawaka sasa wewe hizi habari za kuufunga mgodi wa north mara umezipata wapi? Kwahiyo unataka kuwaaminisha watu kwamba watu wote wanaoishi nyamongo ni maintruders?

Na wale wafanyakazi wote wa barrick na contractors wanaoishi nje ya mgodi wananchi wa nyamongo hawawaoni na kuwashambulia? unadhani kama wananchi wa nyamongo wanauhasama na kila mtu anayetoka ama kufanya kazi mgodini inakuwaje bado wanaweza kuishi nao mitaani tena wao ndio wanawapangisha nyumba zao? think out of the box!!
 
Wewe ulishafika Nyamongo au unawajua watu wa Nyamongo? Au unaongea kwa kusikiliza maneno ya wanasiasa.
 

Sasa unabisha nini? Risasi ya moto ni last resort. Unadhani mabomu ya machozi, maji ya kuwasha ni kwa ajili ya show? Kazi yake kutawanya watu. Ukitumia risasa ya moto piga mguuni, hiyo ndo principle. Hutaki unaacha. After all, katika incidence za polisi kuuwa raia, niambie moja tu ambapo raia walikuwa na mabomu au bunduki. Anzia issue ya mwembechai, njoo ya uchaguzi zanzibar, nenda ya cdm arusha, ya ally pale morogoro na malizia na hii ya juzi huko iringa.
 

Kwahiyo unataka kutuambia kwamba watu wa nyamongo hawapati madhara yoyote wakipigwa na mabomu ya machozi siyo? ndio maana juzi polisi wenu wakaamua kumfyatua Daudi Mwangosi watakuwa walidhani kwamba naye ni mtu wa nyamongo!!!
Sijawahi kusikia kwamba wananchi wa nyamongo wako katika mapambano na polisi lakini polisi wanaendelea kuwaua kwa visingizio mbalimbali bila hata sisi wananchi kustuka na kuihoji serikali, sasa tumebaki kupiga majungu na kuwakashfu wana nyamongo na tarime.
 
Wewe ulishafika Nyamongo au unawajua watu wa Nyamongo? Au unaongea kwa kusikiliza maneno ya wanasiasa.

Unaniuliza kufika nyumbani kwetu?
Sasa wewe uliyefika niambie wale wafanyakazi wa barrick na macontractor wanaokaa mitaani nje ya mgodi wanalindwa na nani kama kweli wananchi wa nyamongo ni washari kiasi hicho?
 
Unaniuliza kufika nyumbani kwetu?
Sasa wewe uliyefika niambie wale wafanyakazi wa barrick na macontractor wanaokaa mitaani nje ya mgodi wanalindwa na nani kama kweli wananchi wa nyamongo ni washari kiasi hicho?
Wanaokaa nje ya mgodi wengi wao ni wenyeji wa palepale yaani wamezaliwa palepale.Lakini wawekezaji na viongozi wa mgodi waliotoka nje ya Nyamongo hawakai mitaani.
 
Tatizo wewe ni mwanasiasa.Ukweli unaujua kuhusu watu wa Nyamongo lakini hutaki kuusema.
 
Unaniuliza kufika nyumbani kwetu?
Sasa wewe uliyefika niambie wale wafanyakazi wa barrick na macontractor wanaokaa mitaani nje ya mgodi wanalindwa na nani kama kweli wananchi wa nyamongo ni washari kiasi hicho?

Wewe hujafika Nyamongo.
 

Mwita ndugu yangu, mimi sijasema ABG wanataka kufunga mgodi, soma tena.. nimesema wanataka kuuza kwa wachina na sababu moja wapo ni hasara wanazopata.
Kingine kama umesoma vizuri nimesema intruders ndio wanaosumbua pale, si wananchi wote wa Nyamongo, lakini wanapokuja kuvamia hawa jamaa muda mwingine hufika hata watu 200 -300, lakini siwezi kusema ni watu wote wa Nyamongo. Kwa kifupi Nyamongo kuna tatizo na haswa hao intruders, wewe unataka tu kukataa ukweli na kile wanachofanya intruders sio kitendo cha kuachiwa tu. Mzee unajua mimi kuna workmate wangu walimchinja? Acha kutetea uhuni bwana.
 

Pamoja na ulazima wa wananchi wa nyamongo kunufaika na rasilimali ile kama yalivyo maeneo mengine lakini pia kuna mikataba ambayo barrick wameshindwa kabisa kuitekeleza hasa ile ya miradi ya maendeleo kwa jamii zinazouzunguka mgodi. Katika hali kama hiyo usitarajie wananchi wake kimya huku wakiendelea kuteseka na kushuhudia rasilimali yao ikifilisiwa mbele ya macho yao, na ukumbuke kwamba watu hawa miaka yote wameishi kwa kutegemea uchimbaji wa dahabu kukidhi mahitaji yao.

Lakini pia usisahau kwamba tofauti na nyamongo, hakuna mahali pengine popote penye mgodi ambapo pameripotiwa barrick kufanya uharibifu mkubwa wa kimazingira kama uliofanyika mto tigite kwa kuruhusu kemikali za sumu kuingia katika mto huo unaotumiwa na wananchi wengi kwa ajili ya mahitaji ya kibinadamu pamoja na mifugo yao, hapa ukumbuke kuna watu pamoja na mifugo wengi sana wamekufa kutokana na sumu zilizotiririshwa kuingia mtoni humo.
 
Huyu Mwita inaonyesha ni Mwanasiasa ukweli hataki kuukubali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…