Polisi waingilia mkutano wa Chadema jimbo la Mtama


Namwelewa sana bwana Kigaila. Huyu simwoni akiongea maneno matupu.
 
..kuna kipindi Ccm walikuwa wakisema Chadema ni chama cha msimu. Kinaibuka na kufanya siasa wakati wa uchaguzi tu.

..sasa Chadema wamebadilika wanataka kufanya mikutano muda wote, Ccm wanatumia Polisi kuzuia mikutano hiyo.

Duh..
Policcm wanakera sana. Wapo bize na siasa za ccm🙄
 
Ifike mahali,jeshi la polisi lisitumike kisiasa,ninaamini kuna polisi wengi tu,hawapendi wanavyoamriwa na wakubwa wao ambao ni wanufaika wa mfumo.Leo hii haohao polisi,taarifa zinasambaa kua wako kwenye kikokotoo kinachowaumiza,na wanaowaumiza ni haohao wanasiasa,halafu mwishowe wanatumika kulinda wanasiasa na maslahi yao,siyo fair.Mbona Uhamiaji,JW,TISS,hawatumiki waziwazi hivi,polisi wa chini waonyeshe hawatendewi haki,wasitegemee wakubwa wao,kwani wakubwa wao hawawezi kuwasemea vyema,kwani ni wanufaika wa mfumo.
 
Mzee ulomquote ndo alivuruga mchakato wa KATIBA mpya kupatikana ktk uongozi wake.
Bora hata yeye aliweza kusema kuhusu ccm kuacha kutegemea kutumua jeshi la polisi.
 
Ukiamini mwanasiasa yoyote, maisha yako umeyaweka rehani.
 
Bora hata yeye aliweza kusema kuhusu ccm kuacha kutegemea kutumua jeshi la polisi.
Ndo huyo huyo anatukejeli kuwa suala la kudai Katiba mpya ni upepo tu Eti utapita.

Tanzania tunapambana na adui tusiemjua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…