Polisi waishiwa mabomu ya machozi maeneo ya Mjimwema (Kigamboni) na kukimbia!

Polisi waishiwa mabomu ya machozi maeneo ya Mjimwema (Kigamboni) na kukimbia!

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Posts
899
Reaction score
1,103
Leo wa kazi wa mji mwema kigamboni walifunga barabara baada ya kuamriwa kuondoka kwenye eneo la machimbo ya mawe na wananchio hawa kugoma, jambo hilo la kugoma lililazimisha polisi kutumia mabomu kama kawaida yake, ila la kushangaza polisi wameishiwa na mabomu hayo na kukimbia kusikojulikana baada ya wananchi kuwazidi nguvu.

kwasasa jeshi la jwtz limewasili maeneo hayo na linaondoa matairi yalikuwa yamechomwa barabarani, kuwasili huko kwa jeshi hilo kumewafanya wananchi kutulia ila wapo maeneo hayo hayo ya tukio.

UPDATE


KWATAARIFA ZA AWALI ZINASEMA MWANANCHI MMOJA AMEPIGWA RISASI YA MGUU NA MWINGINE AMEPATA AJALI YA KUGONGWA NA PIKIPIKI WAKATI AKIWA KWENYE HEKA HEKA ZA KUJIOKOA. ENDELEENI KUFUATILIA KUPITIA HAPA NITAWAJUZA KILA KITU KINACHOENDELEA NIMEMTUMA KATIBU WA CHAMA WA JIMBO LA KIGAMBONI KWENDA ENEO LA TUKIO ILI CHAMA KIWEZE KUAPATA TAARIFA KAMILI NA SAHIHI ISIYOCHAKACHULIWA.

Kwasasa RPC wa TEMEKE aamuru gulio la Mjimwema kigamboni kufungwa Gulio hilo hufanyika kila siku ya J4, Vijana zaidi ya 12 wakamatwa. kwasasa bado hali ni tete Police wamerudi eneo la tukio. wananchi wapo pembezoni huku wakisikika wakisema hapa kitaleweka tu, ni lazima serikali itusikilize wananchi tunataka nini. endelea kufuatia tukio hili kupitia hapa.
 
hayo machimbo yako nje na ule mradi wao wa mji mpya?
 
Naanza kukubaliana na wale waliosema wanajeshi wanatakiwa sasa waende vitani kwasababu wanagharamiwa tu na pesa za walipa kodi, kama hawafanyi kazi yao,sasa ndo wanatumika dhidi ya wananchi?Kazi ya jeshi ni kulinda mipaka ya nchi si ku police,nchi haiko vitani yote hayo ya nini?
 
Asante kwa taarifa mkuu, nafikiri walikuwa wajifua kwa ajili ya 2015
 
Leo wa kazi wa mji mwema kigamboni walifunga barabara baada ya kuamriwa kuondoka kwenye enero la machimbo ya mawe na wananchio hawa kugoma, jambo hilo la kugoma lililazimisha polisi kutumia mabomu kama kawaida yake, ila la kushangaza polisi wameishiwa na mabomu hayo na kukimbia kusikojulikana baada ya wananchi kuwazidi nguvu.

kwasasa jeshi la jwtz limewasili maeneo hayo na linaondoa matairi yalikuwa yamechomwa barabarani, kuwasili huko kwa jeshi hilo kumewafanya wananchi kutulia ila wapo maeneo hayo hayo ya tukio.

Hii inadhihirisha kuwa kwa sasa Watanzania wamechoshwa na hizi harakati za Polisi za kupiga watu mabomu kila kukicha!

Kwa maana nyingine wako tayari kwa lolote. Acha na hao JW waje na vifaru,risasi na SMG zao watapiga risasi zitaisha na mwisho watakimbia. Huo ndiyo utakuwa mwanzo wa kuikomboa nchi hii iliyo chini ya Mafisadi wa Chama cha Majambazi. Kila kitu kina mwanzo na mwisho wake.

CCM wanapotamba kuwa watatawala nchi hii milele bila shaka wanajidanganya.
 
Hata mwanao kama kila kosa unamtanga mwisho anajenga Usugu! Hii ni dalili kuwa wabongo wameanza kujenga Usugu wa Mabomu ya machozi!
 
kweli hawa polisi na wanajeshi waende vitani maana wanahamu.si wawapeleke somaria wakawasaidie wakenya.
 
Wanajeshi badala ya kulinda mipaka yetu mpaka Malawi wanatangaza kuwa ziwa nyasa ni mali yao kwa 100% wao wanakuja kuwatumikia mafisadi.
 
Nadhani hizo ni salaamu maalumu, wakati wa fidia za kuupisha mji mpya itabidi Serikali ijipange vilivyo.
 
Wamezidi kuwa wengi mjini hata makambini hawapajui siku hizi, full kuleta fujo mjini yu. Hatuombi vita lakini bora itokee waende huko ili wapunguze nghasia kwa wananchi mijini!
 
Jeshi linajidhalilisha na kujiondolea heshima kwa umma
Kwani tuna jeshi?.
Jeshi gani linapigana na wanachi wasio na silaha? Tuna maPolisi wanaotumia sare tofauti tofauti!.
 
Back
Top Bottom