Polisi walioua mfanyabiashara Mtwara wameshachukuliwa hatua za haraka kama panyaroad?

Polisi walioua mfanyabiashara Mtwara wameshachukuliwa hatua za haraka kama panyaroad?

sanalii

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,639
Reaction score
5,767
Najua watanzania wengi ni wabinafsi hawajali haki za wengine na wengine hawafahaumu,lakin Nchi haiwezi kua na amani kama kutakua na double standard na dhulma kiwango hiki.

1. Kama nchi imeamua kushughulikia uhalifu kwa kuua basi tuanze kupewa taarifa ya akari waliohusika na mauji ya kijana mfanyabiashara alieuwawa mikononi mwa polisi kule Mtwara, ule pia ni upanja road

2. Kama mmeamua nchi iwe chamba la bibi basi iwe hivyo kila mtu ajilinde mwenyewe, lakini sio kuua panyaroad wa m mtaani theni unaacha panyaroad kwenye jeshi la polisi

Wale walioua mfanyabiashara walichukuliwa hatua gani za haraka?
Yule kijana hamisi kama yumo na mtoto akikosa malezi akatafuta mbinu mbadala kutafuta riziki chanzo kitakua ni nani?

Sitetei panyaroad ila sipendi panyaroad walioko jeshi la polisi wanavyolindwa.

Kama mmeamua kufata haki basi hata hao panyaroad wa temeke na mbagala wapelekini mahakamani, sio mseme mzazi asipoona mwanae akamtafute central au mortuary
 
Wale panya road wa Ntwara wana idhini ya ccm, usifananishe na hao wa Dar. Kesi itachukua muda mrefu, ili wadanganyika muwe mmesahau, mwisho wa siku wataachiwa.
 
Yaani hii nchi Ina cold cases nyingi mno, na mbaya zaidi hatuna hata ,wapelelezi waliostaafu, investigative journalists, investigative pathologists ambao wangejitolea kuzifuatilia hizi cold cases, kesi ya Akwilina, ni moja ya mfano halisi wa cold case ambayo mimi ninaamini haikuleta justice to the family, Ile family mpaka leo haina closure hasa nini kilitokea in the last minutes za mpendwa wao, murders in uniforms bado wana roam mitaa yetu na kujifanya wanyenyekevu kwenye nyumba za ibada kumbe ni cold blooded killers,but ipo siku nchi hii itajua nini hasa kilitokea kwa watanzania wenzetu waliouliwa na watu tuliowapa wajibu wa kutulinda.
 
Nchii hiii ina panyaroad wengi kuanzia serikalini,bungeni,mahakamani,polisi n.k
 
Back
Top Bottom