Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Polisi wamemaliza kufanya upekuzi nyumbani kwa Meya wa zamani wa Ubungo ambaye pia ni Kada wa CHADEMA, Boniface Jacob ambaye amekamatwa na Polisi jioni leo akiwa maeneo ya Sinza na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar es salaam leo September 18,2024 kisha baadaye kwenda nae nyumbani kwake Msakuzi Jijini Dares Salaam.
Upekuzi umeanza saa tatu kasoro usiku na kumalizika saa sita kasoro usiku huu ambapo kwa sasa Boniface anarejeshwa tena Oysterbay.
Kwa mujibu wa Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Hekima Mwasipu, Boni anatuhumiwa kwa kusambaza taarifa za uongo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ametoa taarifa jioni leo akikiri Polisi kumshikilia Boniface kutokana na makosa ya kijinai anayotuhumiwa nayo “Wananchi wapuuze uongo unaosambazwa mitandaoni kuwa ametekwa”.
PIA SOMA
- NTOBI: Jeshi la Polisi wamefika nyumbani kwa Boniface, hapa Msakuzi kwa ajili ya upekuzi
- Boniface Jacob adaiwa kukamatwa na watu waliokuja na gari aina ya defender. Kamanda Kitwinkwi asema hana taarifa hizo
- Jeshi la Polisi: Tumemkamata Boniface Jacob kwa makosa ya Jinai anayotuhumiwa nayo