Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Maafisa wa polisi huko kaunti ya Murang'a eneo la Kaharati wanamshikilia Mzee mmoja kwa kosa la kupaka rangi matunda ya parachichi kuwahadaa wanunuzi kwenye barabara ya Murang'a kuelekea Nairobi, kwamba tayari wameshakomaa na yanakaribia kuiva.
Katika hali ya kawaida eneo hilo, wanunuzi wengi huwa ni wenye magari na hivyo basi huwa ni nadra sana wateja kuyakagua vizuri mara tu wanapoyanunua.
Kukamatwa kwake kunajiri siku chache baada ya video ya mnunuzi mwanamke kuvuja mtandaoni akitaka polisi kuwachunguza wakulima wa Maparachichi kaunti hiyo kwa kudai ni walaghai, wanaotaka tu kuuza bidhaa zao kwa haraka bila ya kuzingatia uadilifu katika Biashara.
Aidha DCC wa Murang'a Kusini ametoa onyo kali kwa wakulima wa eneo hilo kuachana na Biashara haramu akisema rangi hio inaweza ikawa ni sumu kwa walaji wa Maparachichi hayo.