Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #21
Nadhani kuwekwa ndani kwa lulu ni kwa usalama wake,hata kama ana hatia ama hana hatia.
jamani nyie hivi angekuwa kanumba ni mwanao ungependa kusikia prime suspect yupo free walah angekuwa mwanangu na lulu akaachiwa ingekuwa ama zangu ama zake,aliyekufa hapa ni mtoto wa m2,kwa kweli akae 2 ndani mpaka uchunguzi ukamilike,
Pamoja na kuwa nakubaliana na wewe juu ya uwezo (duni) wa polisi wetu...lakini katika hili la wao 'kumshikilia' Lulu kuhusiana na kifo cha Sk sikubaliani na wewe. Kuna utata mkubwa bado juu ya chanzo cha kifo cha SK...amejiuwa, amekufa, ameuwawa! Kwa maelezo yaliyopo kwenye public mpaka sasa ni kuwa Lulu ndiye aliyekuwa na marehemu na kwa mujibu wa mashahidi (mdogo wa marehemu na majirani) kulisikika 'vishindo' chumba ambacho wapenzi hawa walikuwamo kabla ya SK kufariki. Sasa, katika hali kama hii Lulu ni shahidi muhimu (hasa kama itathibitika kuwa SK ameuwawa) sana katika uchunguzi wa kipolisi na pengine hata ule wa kitabibu. Kuwa wa kwanza kutoa taarifa polisi hakuondoi ukweli kuwa katika hili Lulu anabaki kuwa mshukiwa nambari moja. Baada ya uchunguzi wa awali bila ya shaka anaweza kuachiwa au wakaongezeka wengine.
Marehemu Steven Kanumba
Polisi wetu wameonyesha ukilaza wao kumkamata Lulu ambaye alikwenda kuwaarifu ya kuwa mpenzi wake amedondoka na kufa mwenyewe. Polisi wenye mafunzo stahiki walipaswa kutoa PF, kurekodi kauli za wahusika na kuchukua contacts zao na kuwaruhusu waondoke wakisubiria taarifa ya ukaguzi wa mwili wa mwendazake................................
Kitendo cha polisi kumkamata na kumhusisha na mauaji Lulu ni kumnyang'anya haki zake za asili na za kikatiba za kuwa hana kosa hadi pale atakaposhitakiwa na kosa..................polisi wamemkamata huku hawana ushahidi wowote kuwa kanumba aliuawa na kuwa hiyo ni kesi ya murder na kauli ya kamanda wa polisi aliedai kuwa Lulu atashitakiwa kwa mauaji inathibitisha jinsi jeshi la polisi lisivyojua wajibu wake ndani ya polisi jamii................
katika mazingira ya namna hii nani atatoa taarifa kwa polisi wakati akijua ataanza kubughudhiwa..............na kushukiwa kuwa anahusika na mauaji wakati hakuna ushahidi wowote hadi sasa wa kufanya hivyo.........mtoto wa watu kakoseshwa kula Easter yake kwa sababu ya uzembe na umbumbu wa polisi wetu................kweli tunakazi ya kuwalisha hawa vilaza polisi na familia zao kwa kutubughudhi tu!
Pili, hakuna maelezo kwa nini mdogo wake wa Kanumba - Seth - naye hakukamatwa pia kutokana na maelezo yake mwenyewe kuwa siku nzima alikuwa na kaka yake kabla ya Lulu kuja...................mashaka kama yanaweza kutiliwa kwa Lulu kwa nini watu wote waliokuwapo wakati marehemu yupo hai wasichukuliwe kama ni watuhumiwa bali mdogo wake aonekane hana hatia kama siyo ubaguzi wa kijinsia? kauli ya polisi kuwa ni ugomvi wa kimapenzi ndiyo uliomwuuwa unazidi kulidhalilisha jeshi la polisi kwa kufikia hatma ya swala lenyewe hata kabla ya kusubiri maelekezo ya taarifa za kitabibu...............kutoka Muhimbili.......hii sasa ni aibu kwa jeshi la polisi....................na yaonyesha kuna watu wengi wamefungwa kutokana na huu uzembe wa kufikiri wa polisi wwetu........
.............katika khali ya kawaida Lulu alitaka kuishia lakini ni mwendazake ambaye alikuwa anamzuia na yaonekana alikuwa ana nguvu zaidi ya kumzuia pale alipoweza kumrudisha chumbani na kufunga mlango wa chumba..........................watu hudondoka tu kwa viungo ndani ya miili ayo kushindwa kutekeleza majukumu yake..........viungo hivyo ni kama moyo, maini, figo, bandama n.k na hata ubongo waweza kushindwa kufanya kazi na mtu akadondoka chini na kupata majeraha ambayo mbumbumbu wetu wa polisi hawana zana za upembuzi yakinifu hata kusema hakuna kesi ya aina yoyote ile hadi pale watakapopata taarifa ya post-mortem kutoka kwa madaktari Muhimbili.................................
polisi wamwachie binti akale sikuukuu au vinginevyo wajiandae kumfidia kwa usumbufu na udhalilishaji waliomsababishia...................
acha wafu wazike wafu wenzao!! yesu aliposema hivi watu walibaki wamemtolea macho bila kuelewa kwa nini alisema hivyo. Poleni wafiwa.
una act as if wale wanaitwa ma bush lawyer
But let me tell u one thing........... this is not about hisia na mawazo yako or something like that.............. this is a criminal procedure.
For now on she's innocent until proven guilty
Kumbuka she is only one who knows what happening to him, hii inamaana she is a primary suspect
naunga mkono sana LULU kuachiwa ila baada ya kujilidhisha usalama wake,kifo cha kanumba kwa kusikia na kusoma magazeti,kuna mambo kaza ya kuangalia1.baada ya kuangua hawa ndugu waliokuwa karibu yake wangemkimbiza hospital haraka inawezekana alipata kitu kitwacho contution ,pia position aliyokuwa amelala haikuwa sawa inawezekana kabisa2.dokta wake hakuwa na maamuzi ya haraka unaposema njoo unichukue ili uje kwenye tukio muda utakao pita kwa maisha au breathing iliyo diffult mara nyingi hautamkuta,atakufa tu.mwendo wa manurse na madocta huwa ni chap chap sasa huyu ni dr zoba3dada yake pia hawakuwa na uamuziwa haraka wa msaada4.kanumba kama alikuwa amekunywa pombe na akaingia kwenye hasila saikolojia inasema huwezi kumaintain normal condition.na alipoaguka huwezi ku-control ukiwa kwenye contution5.kanumba kafa kwa umasikini wa nchi yetu,umasikini wenyewe ni fikira na infrastracture ya kufika kwenye huduma.
mbona unajikaanga kwa mafuta yako......if she is innocent why apprehend her?...........kuhusu kuwa Lulu ni prime suspect for what.........................hivi polisi wamesema wamekiri kuwa hawajui kuwa kama kuna mauaji au ni kifo cha maradhi ya kawaida......................sasa prime suspect kwa kosa lipi?...........polisi lazima watangaze kuwa hii ni homicide wakishindwa kufanya hivyo mtuhumiwa lazima umwachie huru hadi pale ushahidi wa kumkamata na kumshitaki utakapopatikana................fikiria wewe uko kwako na mmoja wenu kafa halafu polisi wanakufanyia unyama huu wa kukukamata hata kabla hawajapata post-mortme report itakapokuja na kuthibitisha ni ugonjwa wa moyo ndiyo uliomwuuwa lulu anafidiwa vipi kwa usumbufu na kudhalilishwa na hawa polisi bomu?
ni vyema wakamwacha binti wa watu akale sikukuu yake.....................mwuuaji huwezi kumjua kwenye mazingira haya bila ya afya ya kanumba kueleweka........hadi hivi sasa polisi hawana ushahidi wowote sasa kwa nini wahisi kuna mauaji?
Hivi mkuu unaonge kwa kufuata sheria ama unaongea kwa matakwa yako binafsi?
nadhani unaelewa kuwa Tanzania nzima inaelewa kuwa Lulu ndie aliyekuwa na marehemu hadi dakika za mwisho hilo halina ubishi,hata kama Lulu hausiki na kifo hicho ni lazima awekwe ndani hii ni kwa ajiri ya usalama wa Lulu mwenyewe
kwani kanumba alikuwa na washabiki wengi na ana ndugu ambao wameondokewa na mpendwa wao,kwa hiyo kama itatokea polisi wakamwachia Lulu na akashambuliwa na kupoteza maisha yake watu wa kwanza wa kulaumiwa ni polisi,kwa hiyo polisi wanafanya kazi zao kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni
la sivyo wewe kama wewe uwe mlinzi wa Lulu CHOCHOTE kitakachotokea juu yake wewe ndie utakae husika
kukamatwa kwa lulu ni kwa usalama wake,ingawaje mashitaka pia yatakuja baada ya uchunguzi
crime scene is contaminated pale ambapo dakitari aliruhusu mwili uondolewe kabla ya polisi kufika na dakitari wala Seth hawakamatwi.....................waombelezaji akiwemo JK wameshiriki kwenda kuvuruga ushahidi kutokana na polisi kutolifunga eneo la crime scene ............sasa Lulu atatendewa haki kweli?