KERO Polisi wana matumizi makubwa na mabaya ya nguvu katika ukamataji wa bodaboda Dar es Salaam

KERO Polisi wana matumizi makubwa na mabaya ya nguvu katika ukamataji wa bodaboda Dar es Salaam

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
Oct 7, 2024
Posts
9
Reaction score
10
Mimi ni bodaboda ambaye kwa namna moja ama nyingine nimekutana na mikasa ya aina mbalimbali barabarani kama ajali, kuibiwa pamoja na kadhia ya kukamatwa na Askari wa Usalama barabarani kwa makosa mbalimbali ya barabarani.

Ni kweli ninakiri mara kadhaa nimekuwa nikivunja sheria za barabarani muda mwingine si kwa kupenda; Kwa mfano mimi nina leseni ya udereva, pikipiki yangu ina bima nina kibali cha LATRA pia ninavaa Kofia ngumu (Helmet) pamoja na viatu.

Sasa muda mwingine ninakutana na abiria kwa mfano anaenda Mbagala kutoka Kariakoo labda sasa ukimwambia nauli ni TZS 5,000 wengi hawana uwezo kwa hiyo unaona ni bora umpakie kwa TZS 2,000 umuunganishe na abiria mwingine wa TZS 2,000 ili angalau uwe na 4000 uweze walau kupata riziki.

Picha linakuja pale unapokutana na Askari hususan Askari Kanzu au Sungusungu anakuja anachomoa funguo anataka umpe TZS 5,000 au TZS 10,000 la sivyo anakupeleka kwa Askari akuandikie vyeti viwili. Kama hiyo haitoshi sometimes unaweza kudhalilishwa barabarani kama kijana siku nilipigwa vibao na Askari wa kike pale kwa Aziz Ally namkumbuka hadi jina. Nilipata hasira lakini nilijizuia kumpiga kwa sababu alikuwa na sare.

Juzi pia wakati napita Mtongani Askari wa Usalama barabarani aliona mbinu rafiki ya kunikamata ni kurusha chuma kirefu kwenye tairi la mbele ili kishike spoku za tairi ili pikipiki isimame.

Hii sio sawa ni kweli bodaboda sometimes tunavunja Sheria kama nilivyoeleza hapo juu lakini ukamataji unaotumika na Askari sio mzuri atakuja kuumiza mtu, muda mwingine tunabeba ndugu zenu pia, tumesoma na tumeona tujiajiri huku msituone wajinga pia tuna familia.
 
Back
Top Bottom