ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
MUENDELEZO WA VITISHO NA MATENDO YA UKIUKWAJI NA UVUNJWAJI WA HAKI ZA BINADAMU YANAYOFANYWA NA JESHI LA POLISI NCHINI.
Idara ya Haki za Binaadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi ya ACT Wazalendo Taifa imepokea taarifa mbalimbali kutoka kila pembe ya nchi juu ya Muendelezo wa Vitisho na Matendo/Matukio ya Ukiukwaji na Uvunjifu wa Haki za Binaadamu nchini kutokana na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika Tarehe 27/11/2024. Kama mnavyofahamu Chama chetu kimeshatoa msimamo wa kutotambua na kukubaliana na matokeo ya Uchaguzi huo nchi nzima kutokana na mchakato mzima wa uchaguzi kuvurugwa kwa kiwango ambacho kimepora madaraka ya wananchi kuchagua Viongozi wao wanaowataka katika maeneo yao, Tumeshuhudia matumizi makubwa ya Vyombo vya dola-Jeshi la Polisi katika mchakato huo, na kupelekea Wanachama na Viongozi wetu wa maeneo mbalimbali kukamatwa, kupigwa, kuteswa na kuumizwa vibaya sana kuliko chama chochote kile, hii inatokana na ukweli wa jinsi tulivyojipanga. Kudhamiria, kuwa na Dira (Ilani bora ya Uchaguzi), na Wagombea bora kuweza kushiriki katika uchaguzi huo, kukua kwa kasi na ukubwa wa taasisi yetu katika kuziongoza siasa za upinzani hapa nchini, na ACT Wazalendo kuwa Mbadala wa Uhakika wa siasa za Tanzania.
Kutokana na hilo Chama chetu kumeshambuliwa vya kutosha, na baadhi ya matukio hayo tumeshawahi kuyatolea taarifa kwa umma. Kumekuwepo na muendelezo wa matukio mfano wa hayo yakitendwa na Jeshi la Polisi na Chama kimeona ni vyema kuujulisha umma wa Watanzania juu ya suala hili kama ifuatavyo;
KUKAMATWA KWA WANACHAMA WETU SABA (7) KATA YA RUHUHU, WILAYA YA LUDEWA MKOANI NJOMBE;
Kata hii ambayo inaongozwa na Diwani anayetokana na Chama chetu ACT Wazalendo uchaguzi ulivurugwa na kunajisiwa kama ilivyokuwa kwa maeneo mengine. Mara baada ya kuapishwa Viongozi waliowekwa madaraka kwa nguvu za dola na Wasimamizi wa Uchaguzi, mnamo Tarehe 3/12/2024 majira ya usiku watu wasiofahamika walisambaza barua za vitisho katika ofisi mbalimbali za wilaya ya Ludewa Kata ya Ruhuhu. Barua hizo zilibandikwa ofisi ya Mtendaji Kata, ofisi ya Mtendaji Kijiji, ofisi ya Chama Cha Mapinduzi, na ofisi ya Chama chetu ACT Wazalendo.
Juzi usiku askari Jeshi la Polisi wamevamia katika Kata ya Ruhuhu na kukamata watu hovyo kwa kuvunja milango ya nyumba za Wananchi na kuingia ndani watu wakiwa wamelala na familia zao. Askari wa Polisi limewapiga Wananchi na zaidi kuwalenga wafuasi wa Chama chetu huku wakilazimisha Wanachama wa ACT Wazalendo kuvaa sare za Chama kabla ya kuondoka nao toka Kijijini hapo na wale waliogoma kuvaa sare za Chama waliendelea kuwapiga sana. Baadhi walilazimika kuhama majumba yao na akinamama na watoto wakikimbilia porini kuogopa kupigwa na Askari wa Jeshi la Polisi. Katika kadhia hiyo waliokamatwa bila ya utaratibu wa kisheria kwa tuhuma hizo ni Mwanafunzi wa Kidato cha nne Ndg. Henry Henry, Ndg. Isack Njelekela, Ndg. Joseph Nyenyembe, Ndg. Philolian Kalanda, Ndg. James Lukuwi, Ndg. Solomon Mapunda, na Ndg. Alois Nyimbo.
KUKAMATWA KWA VIONGOZI, NA WANACHAMA WETU KUMI (10) KATA YA KAGUNGA, JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI NA ISHIRINI (20) KATA YA RUGONGWE, JIMBO LA MUHAMBWE WILAYA YA KIBONDO, MKOANI KIGOMA;
Viongozi na Wanachama wetu 10 wameshikiliwa na Jeshi la Polisi toka Tarehe 27/11/2024 kwa tuhuma za kuharibu nyaraka za Mtendaji wa Kijiji cha Kaguna katika Kitongoji ambacho ACT Wazalendo tumeshinda, kati ya waliokamatwa saba (7) ni Wanawake wenye watoto wadogo (Rehema Shabani Jackob na Amina Juma Kapomo) Aidha zaidi ya Wanachama na Viongozi wetu 200 wamekimbia makazi yao katika Kata za Pamila, Matendo, Nkungwe, Mgaraganza na Kigoma Mjini kutokana na kuogopa vitisho, kupigwa na kukamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi.
Baada ya ufuatiliaji mkubwa uliofanywa na Viongozi wetu wa Chama Kigoma jana na juzi walifanikiwa kuwawekea dhamana na kutakiwa kurejea tena kituoni hapo Tarehe 9/12/2024. Waliokamatwa ni Ndg. Nassibu Zenda (Mkapa), Ndg. Tulenao Issa, Ndg. Zainabu Yazid (Mwanafunzi Kidato cha III), Ndg. Mwanajuma Bemee Haruna, Ndg. Sikujua Jumanne, Ndg. Siyawezi Mussa Sungumila, Ndg. Ismail Maliki, na Ndg. Kakoti Shabani Ntahugumba ambae ameumizwa na kuteswa sana yeye pamoja na mkewe ambae ni mjamzito, licha ya kuwa mikononi mwa Polisi aliendelea kupigwa wakati wa mahojiano huku wakimwambia kuwa wewe ndio unajifanya ACT Kindakindaki? Kupewa vitisho vya kufungwa maisha nk, Pamoja na yote wakati wa kutoka kwake ameibiwa viatu vyake vipya alivyovikabidhi wakati anaingizwa mahabusu na kulazimikaa kurudi nyumbani pekupeku.
Aidha, Wanachama na Viongozi wetu 20 wa Jimbo la Muhambwe, Wilaya ya Kibondo, Kata ya Rugongwe tawi la Kichananga wamekamatwa usiku wa Tarehe 28/11/2024 na Jeshi la Polisi na kupelekwa Kituo Kikuu Cha Polisi Kibondo, wakati Kifura kuna kituo cha Polisi. Hii yote ni kutaka kuwatesa na kuwapa usumbufu wa gharama za nauli na kuwapotezea muda wa kwenda na kurudi kuripoti kisa ni kwa nini waliwazuia usiku wa kuamkia uchaguzi CCM wasitoe Rushwa kwa Wananchi.
KUKAMATWA KWA DIWANI WETU WAKA KATA YA RUNGWE MPYA AMBAYE PIA NI KATIBU WA JIMBO LA KASULU VIJIJINI –MKOA WA KIGOMA NDUGU JONAS ABEL KAJA;
Diwani na Kiongozi wetu wa Jimbo ameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za eti kuhusika na kumwagia tindikali Katibu wa CCM na Mkewe hivyo kushtakiwa kwa kosa la Kujeruhi katika kituo cha Polisi Kasulu Mjini, (Mlimani) na kupewa namba ya jalada la kesi KAS/IR/3459/2024. Baada ya kufikishwa Mahakamani amepewa dhamana anaendelea na kesi.
MATUKIO MENGINE NI PAMOJA NA;
Kupigwa kwa Mawakala wetu wa Uchaguzi Vituoni, Kituo cha Ngajengwa Kata ya Igima Jimbo la Mlimba, Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Mara Jimbo la Musoma Vijijini kitongoji cha Kilimani nk.
Kukamatwa kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Mwenyekiti wetu wa Mkoa wa Songwe Ndugu Ezekia Zambi.
Kupigwa na kuumizwa vibaya na makada wa CCM kwa Katibu wetu wa Jimbo la Igunga Ndugu Elick Yugalila Venance, na mpaka sasa Jeshi la Polisi halijachukua hatua yeyote ya kuwakamata wahusika mbali na kutambulika waziwazi kwa sababu walimvamia barabarani wakiwa na pikipiki za CCM zenye nembo ya Rais Samia.
Kukamatwa kwa Katibu wetu wa Jimbo la Ulyankulu ndugu Zakaria Sangijo Lugembe, kwa kisa cha kuhoji kwanini majina ya wapiga kura yaliyobadikwa hayasomeki kutokana na CCM kuyamwagia maji.
Mgombea wetu katika Kitongoji cha Siruka, Kijiji cha Sudi Jimbo la Rorya Ndugu Ayubu O. Aguga alikamatwa na Polisi. Katibu wetu wa Mkoa wa Mara Ndugu Karume Jeremiah Mgunda akiwa njiani kutoka kumfuatilia Kituo cha Polisi Utegi alivamiwa na Vijana watano (5) wa CCM na kupiga vibaya RB –UGI/IR/580/2024.
Kufanywa kwa uharibifu wa mali za Mgombea wetu na kumpiga sana Ndugu Muhidin Kimbukwa kumpora simu pamoja na Ndugu Nuran Ungando. makundi ya makada wa CCM Wamempiga binti wa Mgombea wetu wa Kijiji cha Mgomba Kati (Nyamsango) Bi.Shani Mbonde mpaka damu imevilia tumboni na kulazwa katika kituo cha afya Ikwiriri-Rufiji. Iliporipotiwa Polisi, Jeshi la Polisi limeshindwa kuchukua hatua na wakawashauri makada waliofanya hivyo waende Hospitali wakamuombe radhi, na wao wakafanya hivyo. Hili ni Jimbo la Waziri wa TAMISEMI. Pale tunapotoa taarifa ACT Wazalendo Jeshi la Polisi halichukui hatua ila kwa CCM wanafanya mpaka wanapitiliza maadili ya kazi zao.
Juzi usiku katika Kijiji cha Angalia Wilaya ya Tunduru, Mkoani Ruvuma Askari wa Jeshi la Polisi wamewavamia wananchi na kuwapiga sana na kisha kuondoka na Mwenyekiti wa Kitongoji Ndugu Mohamed Yahya Mpacheni na mpaka jana hajulikani yupo kituo kipi cha Polisi. Pamoja na Mwanachama wetu ambaye pia ni mshindi wa Kitongoji cha Mtogoro Kijiji Cha Angalia Tunduru Kusini, Ndugu Rashid Zuberi Mtogoro alishambuliwa na askari wa FFU kukamatwa na kuwekwa rumande.
LEO wakati najiandaa na Mkutano huu nanyi Waandishi wa Habari nimepokea Taarifa toka Jimbo la Kigoma Kusini, Mwenyekiti wetu wa Kitongoji cha Muyobozi katika Kijiji na Kata ya Mwakizega Ndg. Bilo Juma Hamisi amekamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kuitikia wito wa kufika kituo cha Polisi Ilagala bila kujua kosa lake wala maelezo yeyote. Mwenyekiti wetu wa Kata Ndg. Rashid Rukwiye alipofika kituoni hapo kutaka kujua anashikiliwa kwa kosa gani amefukuzwa na kuambiwa analeta fujo naye atakamatwa na kuwekwa ndani. Hii ndio dhana ya utii wa sheria bila ya shuruti inavyotekelezwa na Jeshi la Polisi.
Suala la Vitisho, na utekwaji wa Mwenyekiti wetu wa Vijana Taifa Ndg. Abdul Nondo sote tunalifahamu.
Nikiainisha haya machache; Matukio ya vitisho, ukamataji, kupigwa, kuteswa na kuumizwa kwa Wanachama na Viongozi wetu nchini ni mengi sana.
ACT WAZALENDO TUNATAKA HATUA ZIFUATAZO ZICHUKULIWE;
1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuingilia kati na kuviamuru Vyombo vya ulinzi na Usalama kuacha mara moja uonevu wa Kisiasa unaoendelea nchini. Kuwazuia na kuwanyima Wananchi Uhuru na Haki ya kushiriki siasa, na kuwa na Uhuru wa maoni, Kujieleza ni kukiukwa na Kuvunjwa kwa misingi ya Haki iliyowekwa na Katiba ya nchi. Iko wapi falsafa ya 4Rs, nini tafsiri ya Amani na Utulivu kwa CCM?
2. Viongozi na Wanachama wetu wote wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi nchini kuachiwa huru bila usumbufu wa kutakiwa kuripoti vituoni mara kwa mara na kama wana tuhuma walizozithibitisha wafikishwe Mahakamani waweze kujitetea kwa mujibu wa Sheria.
3. Jeshi la Polisi liwakamate makada wa CCM waliofanya uhalifu na kuripotiwa mbele yao na waache kutenda kazi zao kwa upendeleo wa Kisiasa, Jeshi la Polisi si mali ya CCM, ni la Watanzania wote ambao wanalipwa na kuhudumiwa na kodi za Wananchi wote bila kujali itikadi za Vyama.
4. Jeshi la Polisi liache vitendo na mwenendo wa kupandikiza chuki za kisiasa miongoni mwa raia, kutoa vitisho, kutesa na kupiga, kuwabambikizia kesi Viongozi, Wanachama wetu na Wananchi kwa ujumla. Kama hawataki kukosolewa watende Haki na au CCM wafute mfumo wa Vyama vingi nchini. Hatuwezi kuwa na Taifa ambalo msimu wa uchaguzi ni muda unaotumika kuua, kuteka, kutesa, kupiga na kuwabambikizia kesi Wapinzani.
5. Tunalitaka Jeshi la Polisi kuacha kuwalenga (Targeting), kuwasumbua kuwakamata na kuwashikiria Wanachama, Viongozi na Wagombea wetu waliosimama Imara kupinga dhulma kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
6. ACT Wazalendo tunaunga mkono Hotuba ya Kiongozi Mstaafu wa Chama aliyoitoa Kigoma juu ya Jeshi la Polisi na Siasa, pamoja na tathmini na maoni ya Jaji Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Pinde Warioba aliyoitoa hivi karibuni juu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
7. Tunawataka Viongozi, Wanachama wetu kuendelea na msimamo wa kupigania Haki na Demokrasia nchini bila kukata tamaa, kuogopa vitisho vya watawala na vyombo vya dola na kutekeleza msimamo wa Chama kwa vitendo kutokana na matokeo ya mchakato wa uchaguzi uliovurugwa kwa makusudi na Wasimamizi wa Uchaguzi na Vyombo vya dola.
8. Tunatoa wito kwa Wadau mbalimbali wa siasa nchini, Jumuiya ya Kimataifa, Wasomi na Viongozi Wastaafu wanaoheshimika kutokubali kuipeleka nchi yetu katika vurugu za kisiasa, ubinywaji wa Haki, Uhuru, Demokrasia, na uvunjifu wa Katiba ya nchi kwa maslahi na ubinafsi wa kikundi cha watu wachache hapa nchini.
ACT Wazalendo tunaamini kuwa matumizi ya Vyombo vya dola, vitisho, kupiga Wananchi, Utekaji, mauaji, kubambikiza kesi kamwe haitaweza kuwanyamazisha Watanzania na Wana-ACT Wazalendo katika kudai Haki, Usawa, Demokrasia, Tume Huru ya Uchaguzi na Mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi na Madai ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakayopatikana kwa ridhaa ya Wananchi wenyewe na kuakisi mfumo wa siasa za Vyama vingi nchini.
Mbarala Maharagande,
Naibu Katibu wa Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi,
ACT Wazalendo Taifa.