Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,199
Ndugu zangu,
Naamini kila mtanzania hivi sasa ni shahidi wa matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza nchini kwa kuwahusisha polisi. Pamoja na mfululizo wa polisi kuua watu kwenye mikutano ya CHADEMA, yakiwemo mauaji ya Arusha, Morogoro, Mwangosi na mfululizo wa kuwapiga mabomu na kuwakamata wanachadema wasio na hatia, bado hivi mapema tumesikia jinsi ambavyo polisi wamevamia mkutano wa CHADEMA huko Mabibo na kujeruhi watu.
Kwa tafsiri yangu polisi hawafanyi haya kwa bahati mbaya. Ni dhahiri kwamba polisi pia wameichoka sana serikali ya JK, lakini kwa kuwa hawana namna ya kuipindua basi wanaamua kuwapandisha hasira wananchi ili hatimaye waseme yatosha. Huu uonezi, ubabe na ukatili uliopita kiasi wa polisi kwa raia ndiyo uliomng'oa Rais Ben Ali wa Tunisia. Kwa hakika mbinu kama ile ya Tunisia naona ndiyo inatengenezwa hivi sasa hapa Tanzania kupitia jeshi la polisi.
Hawa watanzania hawataweza kuvumilia kuzika ndugu zao kila siku, hawataweza kuvumilia kuuguza ndugu zao kila siku, hawataweza kuvumilia kuishi katika hali ya ukiwa na ujane eti kwa kuwa tu ndugu zao wamekamatwa na kufungwa na polisi kwa makosa ya kusingiziwa. Hawatavumilia kuona ndugu zao wanauliwa na kumwagiwa tindikali halafu kesi ikifika polisi inapotezewa tu. Hawatavumilia kuona ujambazi na uharamia unaofanywa mitaani kwetu ukiendelea huku jeshi la polisi likiwa linaonekana kutokujali.
Ukivamiwa na majambazi, ukapiga simu polisi daima watafika dakika tano hadi kumi mara tu baada ya majambazi kutoka. Jambo ambalo linaashiria kwamba polisi na majambazi daima huwa na mawasiliano ya karibu juu ya kile kinachotupata. Mambo haya watanzania hawataweza kuendelea kuyavumilia. Definitely watajiunga kuikataa serikali hii isiyoweza kuwalinda, inayowaua, inayowaumiza, inayofunga bila kosa, na inayokandamiza haki zao.
Si rahisi sana kwa jeshi la polisi kufanya mambo ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kiasi kikubwa hivi katika hali ya kawaida. Kwa hakika jeshi la polisi linafanya haya ili kuwaudhi watanzania, ili watanzania wakose uvumilivu waseme sasa yatosha. Ni hakika kwamba jeshi la polisi limeichoka serikali hii, lakini halina namna yoyote ya kuwaambia watanzania kwamba walichagua serikali mbovu, kilichobaki ni kuwachapa hawa watanzania hadi waichukie serikali yao, na kuingia barabarani kuitaka itoke.
Mimi si nabii, lakini tukijifunza kutoka kwa wenzetu, basi tutajua ni nini kinachofuata katika nchi yetu iwapo vitendo hivi vya kikatili vitaendelea.