Polisi Wasababisha Vifo vya Wanafunzi Sumbawanga

Keykey

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2006
Posts
3,251
Reaction score
747
Mh. Pinda unayajua haya? Kuna hatua zimechukuliwa au hadi iundwe tume nyingine kuchunguza?

Inapofikia polisi tunaowatarajia kutulinda wanaua watoto wetu? Tunasuburi kuona waliohusika wakiwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

 
ni masikitiko makubwa sana kwa haya yaliyotokea. Mwenyezi Mungu awarehemu vijana hawa Inshaalah Amin.
 
Serikali iache kutumia maguvu mengi kuliko inavyopaswa. kwanza siyo sifa!
mabavu, mabavu bila kuangalia athari ya mabavu hayo ni ishara za woga na wala siyo busara.
Tunataka vyombo vyetu vya usalama viwalinde wananchi na visitumiwe na wanasiasa woga, wasiojiamini kutatua matatizo ya wananchi. wanasiasa wanaotanguliza mabavu mbele halafu fikra baadae ni hatari sana popote pale duniani
 
Jamani hawa polisi vipi ? Mwema yuko wapi ? Anategemea kufanya nini ? JK unasemaje ? Mbona Tanzania ya JK ina mashida mengi hivi ?
 
Jamani hawa polisi vipi ? Mwema yuko wapi ? Anategemea kufanya nini ? JK unasemaje ? Mbona Tanzania ya JK ina mashida mengi hivi ?

Bado sijaona Polisi wamehusika visi katika vifo vya wanafunzi hawa. Ninachohisi ni labda vurugu zilikuwa kubwa,na Polisi wakaamua kupiga risasi hewani na kutumia hayo mabomu ya machozi, ni katika panic wanafunzi kukimbia na mambo kama hayo ya kuanguka mtoni yakatokea, unless kama Polisi walihusika kuwasukuma huko mtoni, then they should be blamed kwa kusababisha vifo.
May be tupunguze kulalamika tu kila wakati, "Mwema yuko wapi"? "JK unasemaje"? I'm at a loss, how are they involve in this?
Let's say wewe ungekuwa ni hao Polisi katika mazingira hayo, ungefanya nini? Au wewe ni hao wanafunzi, ungefanya nini? Au wewe ni huo uongozi wa shule, ingefanya nini? Au wewe ni..., au, au , au , au.........
Let's think big.

Ni hayo tu.
 
Ni kubaliane na wewe Lizy kwa hayo uliyoysema maana tumekuwa tukilalamika sana lakini tumekuwa tukishudia hata nchi zilizoenselea zimekuwa zikitumia nguvu kila inapobidi tuache kulalamika sana
 
Haya ndiyo yaliyoandikwa kwenye magazeti kuhusiana na fujo hizi.

 
Mm naona waziri wa USARAMA WA RAIA anapaswa kuwajibika kwa hili swala hata MWEMA naye hana budi kuwajibika.
Tatizo la viongozi wetu kung'ang'ania madaraka angalia sasa vijakazi wao wameua nani anapaswa kuwajibika??si wao wakubwa?lazima wawajibike ni aibu kwa polisi jamani/.
 
Ni kubaliane na wewe Lizy kwa hayo uliyoysema maana tumekuwa tukilalamika sana lakini tumekuwa tukishudia hata nchi zilizoenselea zimekuwa zikitumia nguvu kila inapobidi tuache kulalamika sana

Nikidhania unamaanisha nchi zilizoendelea kwenye bold, nakuuliza swali kidogo utaje hizo nchi zilizoendelea ambazo zinatuma polisi wake kufukuza watoto wa shule hadi mtoni na kuwaacha wakafia huko eti kwa sababu wamefanya fujo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…