Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Polisi watatu wamekamatwa nchini Kenya baada ya mmoja wa polisi hao kuonekana akimchapa na kumburuza mwanamke mmoja kwa pikipiki.
Mwanamke huyo anadaiwa kuhusiana na tuhuma za wizi mjini Nakuru.
Mwanamke huyo amelazwa hospitali baada ya kuumia miguuni na mikononi.
Mwanamke huyo amekiambia kituo cha Citizen TV kuwa anamfahamu polisi huyo.
Idara ya Upelelezi ya polisi imesema polisi watatu wamekamatwa na wanaisaidia polisi kwa uchunguzi wa tukio hilo.