Polisi watatu Kenya wakamatwa kwa kumburuza mwanamke kwa pikipiki

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535

Polisi watatu wamekamatwa nchini Kenya baada ya mmoja wa polisi hao kuonekana akimchapa na kumburuza mwanamke mmoja kwa pikipiki.

Mwanamke huyo anadaiwa kuhusiana na tuhuma za wizi mjini Nakuru.

Mwanamke huyo amelazwa hospitali baada ya kuumia miguuni na mikononi.

Mwanamke huyo amekiambia kituo cha Citizen TV kuwa anamfahamu polisi huyo.

Idara ya Upelelezi ya polisi imesema polisi watatu wamekamatwa na wanaisaidia polisi kwa uchunguzi wa tukio hilo.
 
Hawa jamaa tukio kama hili lingetokea nchi nyingine basi wangeandamana.
 
Maandamano lini au kwasababu kaburuzwa mkenya choka mbaya hamna kiki watakayopata hata wakiandamana ee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…