LGE2024 Polisi watoa ufafanuzi kuhusu zoezi la uchaguzi Njombe

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu,

Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe limetoa ufafanuzi kuhusiana na Zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo zoezi hilo lilifanyika tarehe 27.11.2024 mkoani Njombe.

Ni kwamba Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe lilijipanga vema katika kushughulikia matukio yote ambayo yanahusiana na masuala ya Uchaguzi kwa kuwa na askari wa kutosha katika maeneo yote ya kupigia kura na zoezi zima la uchaguzi likwenda salama hapakuwa na matukio makubwa ambayo yalileta taharuki kwa jamii.

Aidha, matukio machache yamejitokeza ambayo hayakuathiri uchaguzi ambapo mgombea mmoja wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA aitwaye Emmanuel Ngelime, miaka 44 mkazi wa Buguruni alikuwa ni Mgombea katika mtaa wa Buguruni lakini wakati zoezi la ukataji wa rufaa na masuala mengine yeye aliweza kuenguliwa lakini siku ya uchaguzi alijitokeza kudai jina lake linatakiwa kuwepo na wananchi wampigie kura lakini Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya rais TAMISEMI ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi walilishughulikia vema na zoezi kuendelea vizuri.

Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe linawashukuru Wananchi wa mkoa wa Njombe kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huu bila ya kuwa na viatarishi vya amani kwa kupiga kura na kurudi nyumbani. Pia Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wale wote ambao hawakuridhika na matokeo basi wafuate taratibu kuliko kuanzisha vurugu na mtu yoyote atakayeanzisha vurugu hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na:
Mahamoud Banga - ACP
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Njombe.

Screenshot_20241128_210323_Instagram.jpg
Screenshot_20241128_210328_Instagram.jpg
 
View attachment 3164583View attachment 3164584
Matamko yote wakosa chadema? Tupangalie tena hapa
 
Polisi wamegeuka wasimamizi wa uchaguzi...ila itoshe kusema mwanzo wa mwisho wa ccm ushafika!
 
Toka mwaka 1995 mnasema mwisho wa ccm umefika ila wenzenu bado wanadunda.
 
Back
Top Bottom