Polisi Waua Raia Arusha

Polisi Waua Raia Arusha

Mfamaji

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2007
Posts
6,630
Reaction score
1,945
Habari za uhakika zinasema kuwa Polisi wameua kwa kuwapiga risasi vijana wawili jana usiku eneo la Kijenge/Mwananama karibu na Mount Meru Petrol Station Kijenge.

Tukio hilo lilitokea baada ya vijana hao kujibizana na mhudumu wa kike kwa kile kilichosemekana ni mhudumu kudaiwa chenji na yeye kudai ameshatoa .Kijana aliyekuwa anayendesha gari alipiga kibao huyo mhudumu na ndipo mhudumu akaita polisi waliokuwa karibu.

Polisi waliwasimamisha vijana hao na kuwaamuru watoke kwenye gari ,ndipo walipowamiminia risasi .As simple as that. More news .....
 
Last edited:
Habari za kuhuzunisha.Polisi wetu wana matatizo sana.Sijui tunaelekea wapi?
 
Ni zao la jamii yetu isiyowajibika,nashindwa kujua polisi huwa wanasoma nini huko CCP moshi,kama anawezafanya unyama na ukatili kama huo.kweli nchi yetu imekuwa kama shamba la wanyama,mwenye ngunvu ndo anaishi
 
Nadhani hao polisi watakuwa wame "assume" kuwa hao vijana ni majambazi kwa vile waliitwa katika kituo cha mafuta, na siku hizi vituo vimekua vikishambuliwa na majambazi.
Ila sisemi kwamba walikua sahihi kufanya hivyo, la. Kwanza ni uzembe, je, hao vijana walionesha ukorofi wowote na kukataa kuwa chini ya ulinzi (arrest)? Je walikua na silaha?
Inasikitisha sana.
 
Nadhani hao polisi hawana akili timamu kwa nini umpige mtu risasi kama jambazi au ameuwa????
 
Siasa chafu, chama kichafu madarakani, viongozi wachafu, watendaji wachafu tabia chafu mitaani.

Usitegemee uhakika wa nidhamu kwa vyombo vya dola wakati wanakuwa na uhakika kuwa wanlinda viongozi wanaotokana na chama kichafu na wanaoshinda uon gozi kwa kutumia mbinu chafu.

Tutegemee mengi zaidi!!!
 
Sidhani kaa kweli polisi wanaweza kuwa wajinga kiasi hiki au wazembe kiasi hiki. Tunahitaji habari zaidi ili tuweze kujua kwa undani. Tuanatakiwa na habari za kutosha kabla ya kumuuliz maswali Mashaa huwezi kujua huenda tuna kina Zombe wengi polisi.
 
Last edited:
Habari za kuhuzunisha.Polisi wetu wana matatizo sana.Sijui tunaelekea wapi?

Kwanini mnawalaumu POLISI ??polisi sio wakulaumiwa uongozi mzima wa nchi yetu ni utata lazima tuwe wakweli sisi wenywe Raia kwanza na tukubali kuwa ni sisi ndio tunaotowa fursa kwanini nikasema hivyo tuangalia tunaowapa zamana za kutuongoza katika miaka nenda na miaka rudi wanatueleza hadisi zile kwa zile na matokeo yake ni yale kwa yale huku sisi tukiwa tunakubaliana na usani wao wanaotulete
 
How reliable is your source???? Sometimes inakuwa ngumu kutoa comments kwenye habari zilizovunjika vipandevipande kama hizi. It will be highly appreciated if you show the source of your informantion to enable free sharing of views. Let us not make the JF a beauty salon please.
 
May God Bless The Dead

From what I remember, God judges the dead!

Is there a breakdown in command and control? The Police are not supposed to shoot to kill without being ordered to do so. Is there a general "shoot to kill order"?

It is, in my view, possible and even desirable, to discuss this issue irrespective of whether the story is true or not. What engagement orders do our officers have?
 
How reliable is your source???? Sometimes inakuwa ngumu kutoa comments kwenye habari zilizovunjika vipandevipande kama hizi. It will be highly appreciated if you show the source of your informantion to enable free sharing of views. Let us not make the JF a beauty salon please.

Japhet.

For God sake this is not a fabricated story. The proof is the dead bodies at Mount Meru Morgue. I personally knew these boys and I am mourning with their relatives at Kijenge . Feel free to comment.

Yule msichana aliyepiga simu ameingia mitini. Polisi hawajatoa statement yoyote hadi sasa, tunaweza kuguess watasema nini.
 
Poleni, msiachie hii kitu iishe kimya kimya. Tumieni vyombo vya habari umma ujue kilichotokea, hao polisi washinikizwe kutoa ukweli na washitakiwe. Bila hivyo wadogo zetu wataendelea kuuwawa, polisi wakiona ni kitu cha kawaida kuwa"trigger happy".
 
Wanajamii lazima hii kitu ya Polisi kuua watu iangaliwe vizuri kwa sababu hawa polisi wa Tanzania wameamua kuua watu kirahisi tu. Kama mtakumbuka kipindi cha Tibaigana tulizoea kusikia kwenye taarifa za habari kila siku kwamba e.g polisi imeyaua majambazi matatu baada ya kurushiana risasi. Baada ya Zombe na wenzake kufikishwa mahakamani habari ya polisi kurushiana risasi na majambazi imeisha kabisa. Tulizoea kumuona kamanda Tossi na mbwembwe zake za ku shoot akiwa na waandishi wa habari akipiga risasi mapipa ya gongo kama ni kitu cha maana sana mpaka unajiuliza kuna haja ya kutumia risasi kutoboa mapipa ya gongo!!! Sasa mtu kama kamanda Tibaigana ambaye alikuwa anapokea taarifa kutoka kwa subordinates wake kwamba kulikuwa na marushiano ya risasi bila ku verify taarifa hizo anatakiwa aende hivi hivi bila hata ya kuwajibishwa. there must be a way ya kuwawajibisha watu wanaofanya mambo kienyeji enyeji tu. Takriban mwaka sasa hatusikii kurushiana kwa risasi kati ya polisi na majambazi. Hiki ni kipindi ambacho kesi ya zombe imeanza kuunguruma. Watu wengi wameuawa. adhabu ya ujambazi au uporaji siyo kifo bila kuhukumiwa na mahakama huru na yenye mamlaka. Kama serikali imeamua kuwashughulikia watu walioliingizia taifa hasara ya fedha basi isiache kushughulikia watu waliowaua raia wa Tanzania bila sababu za kimsingi. Ningekuwa na muda ningefanya research kuona tangu tume ya Kipenka iundwe ni majambazi mangapi yameuwa compared ni miaka mitatu nyuma kabla ya tume ya Kipenka. Waandishi walishughulikie hili
 
Habari za uhakika zinasema kuwa Polisi wameua kwa kuwapiga risasi vijana wawili jana usiku eneo la Kijenge/Mwananama karibu na Mount Meru Petrol Station Kijenge.

Tukio hilo lilitokea baada ya vijana hao kujibizana na mhudumu wa kike kwa kile kilichosemekana ni mhudumu kudaiwa chenji na yeye kudai ameshatoa .Kijana aliyekuwa anayendesha gari alipiga kibao huyo mhudumu na ndipo mhudumu akaita polisi waliokuwa karibu.

Polisi waliwasimamisha vijana hao na kuwaamuru watoke kwenye gari ,ndipo walipowamiminia risasi .As simple as that. More news .....




hii habari imenishangaza siamini kabisa! juzi nilikuwa na shed motika jana naambiwa kauwawa! rest in peace ma bro.
 
Sheria mikononi. hii yote inatokana na umaskini uliyokithiri. Mtu anakuwa na mchungu na mazonge ya kimaisha, sasa akikutana na tukio lolote ndio anapata sehemu ya kutolea machungu yake. Juzi niliona mtu kagongwa na pikipiki alipoinuka akajitizama akaona ni mzima hajaumia mara wakatokea watu wanamwambia jifanye umeumia ili akulipe huyo, wakati kosa na lake mwenyewe alivuka ghafla bila kutizama, lakini watu wameona kwamba pakitokea jambo basi ndio nafasi ya kupunguzia mazonge ya kimaisha, hakuna sababu nyingine zaidi ya umaskini. Jamani Umaskini m-baya sana. Ndio utakuta gari limefanya ajali watu wanampiga dereva tena pengine dereva mwenyewe alifanya juhudi kubwa kuepusha ajali kubwa zaidi. hasira za watu wanazitolea kwa dereva na akikimbia kusalimisha roho yake basi ujue gari litakuwa nyang'anyang'a. watu wanapinguza mazonge ya maisha yao.

Tumuombe mungu atuepushie haya.
 
La maana ni kuhakikisha kuwa suala hili linafuatiliwa ili wenye makosa wawajibishwe ipasavyo
 
Back
Top Bottom