Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kuzima maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam Septemba 23, 2024, baadhi ya askari wameonekana wakizingira ofisi ya makao makuu ya chama hicho Mikocheni.
Mwandishi wa Mwananchi aliyefika katika ofisi hiyo leo Septemba 24, 2024 ameshuhudia askari hao waliokuwa wamebeba silaha za moto wakichungulia madirisha ya ukuta wa chama hicho, huku wengine wakirandaranda nje ya ofisi.
Katika kudhibiti maandamano hayo makada wa Chadema zaidi ya 50 walikamatwa, akiwamo Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti (Bara), Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Godbless Leman na makada wengine.
Alipoulizwa kuhusu uwepo wa askari hao, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema bado wanaendelea na kuimarisha ulinzi kama walivyofanya jana.
"Tunaimarisha ulinzi tangu jana kwenye zile pointi, muhimu hakuna tukio lolote la kijinai lililotokea wananchi wako salama. Polisi kuzingira ofisi za Chadema na wao tunawalinda kama wananchi wengine wa kawaida maana yake hawakawii kusema wametekwa," amesema Muliro.
Akizungumzia hali hiyo, mlinzi wa ofisi hiyo, Kopwe Michael amesema hali ya vikosi hivyo kuzingira katika ofisi hiyo ilianza saa 3:00 asubuhi.
"Zilianza kuja Defender tatu zote zilikuwa zimejaza maaskari ndani yake. Baadaye wakashuka na kuanza kuzingira ofisi yetu wengine wakichungulia ndani kupitia madirisha ya ukutani bila kusema jambo gani wanaangalia au wanatafuta," amesema.