Polisi wazingira ofisi ya za CHADEMA, Muliro adai wanaimarisha ulinzi wasijesema wametekwa

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Siku moja baada ya Jeshi la Polisi kuzima maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam Septemba 23, 2024, baadhi ya askari wameonekana wakizingira ofisi ya makao makuu ya chama hicho Mikocheni.

Mwandishi wa Mwananchi aliyefika katika ofisi hiyo leo Septemba 24, 2024 ameshuhudia askari hao waliokuwa wamebeba silaha za moto wakichungulia madirisha ya ukuta wa chama hicho, huku wengine wakirandaranda nje ya ofisi.

Katika kudhibiti maandamano hayo makada wa Chadema zaidi ya 50 walikamatwa, akiwamo Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti (Bara), Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Godbless Leman na makada wengine.

Alipoulizwa kuhusu uwepo wa askari hao, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema bado wanaendelea na kuimarisha ulinzi kama walivyofanya jana.

"Tunaimarisha ulinzi tangu jana kwenye zile pointi, muhimu hakuna tukio lolote la kijinai lililotokea wananchi wako salama. Polisi kuzingira ofisi za Chadema na wao tunawalinda kama wananchi wengine wa kawaida maana yake hawakawii kusema wametekwa," amesema Muliro.

Akizungumzia hali hiyo, mlinzi wa ofisi hiyo, Kopwe Michael amesema hali ya vikosi hivyo kuzingira katika ofisi hiyo ilianza saa 3:00 asubuhi.

"Zilianza kuja Defender tatu zote zilikuwa zimejaza maaskari ndani yake. Baadaye wakashuka na kuanza kuzingira ofisi yetu wengine wakichungulia ndani kupitia madirisha ya ukutani bila kusema jambo gani wanaangalia au wanatafuta," amesema.
 
Tangu Kuanza kwa Harakati za Maombolezo kwa Wote waliotekwa na Kuuawa, RPC wa Dar, Mtukufu Muliro amekuwa akitoa kauli za Kejeli dhidi ya viongozi wa Chadema na Wanachama wao, Ushahidi wa kejeli zake uko kila mahali.

Sisi Raia wa kawaida hatuna la kumfanya, Bali tunamkumbusha kwamba Cheo alichonacho cha kuteuliwa ni dhamana ya muda mfupi sana, Bila shaka ataondoka na wataingia wengine.

Awe na Akiba ya Maneno

 
Sijui kwa nini baadhi ya watu hupenda kujidhalilisha tu wenyewe bila ya sababu muhimu. Huyu haya majivuno na kejeli yatamsaidia kitu gani hasa!

Hivi yule wa "Kama 1 +2 ni...; yeye kaishia wapi siku hizi maanake hasikiki tena. Nadhani anaitwa Mroto au kitu kama hicho.
 
Dah! Umeandika kwa unyonge sana,pole ndiyo maisha yalivyo usijali!!!
 
Nani alitamba kama Simon Sirro leo yuko wapi ,Muliro aache maneno ya mipasho
Kulikuwa na Gewe,Tibaigana na Kova sasa wako wapi,na Mahita kajenga msikiti Morogoro ana swali yeye na ndugu zake pekee, umesusiwa.
 
Kweli kabisa, wanahitaji ulinzi mkubwa
 
Nani alitamba kama Simon Sirro leo yuko wapi ,Muliro aache maneno ya mipasho
Kulikuwa na Gewe,Tibaigana na Kova sasa wako wapi,na Mahita kajenga msikiti Morogoro ana swali yeye na ndugu zake pekee, umesusiwa.

Mahita alitaka kugombea Ubunge, CCM wakamtema kwenye kura za maoni. Chezea CCM weye.
 
Sisi Raia wa kawaida hatuna la kumfanya, Bali tunamkumbusha kwamba Cheo alichonacho cha kuteuliwa ni dhamana ya muda mfupi sana, Bila shaka ataondoka na wataingia wengine.
 
Baba alikuwa mvuvi mimi nikarizishwa uvuvi nikamrizisha mwanangu uvuvi utagemea nini kwenye shughuli zangu za uvuvi wa asili wakurizishana? Hasa pale mimi na wadogo zangu tuliposhindwa kutoboa kwenye shule za kata? Jibu twende tukavue hata kama mawimbi ni hatari mradi tule tushibe!
 
Wamekuwa wanasingizia kutekwa ngoja walindwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…