Jeshi la Polisi Wilaya ya Same limetangaza kusitisha mikutano ya hadhara ya Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ambayo ilitarajiwa kuanza Novemba 13, 2024.
Hatua hii inakuja kufuatia maagizo kutoka kwa ofisi ya serikali ya mkoa inayozuia mikutano ya hadhara kabla ya tarehe rasmi ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa, ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 20 Novemba 2024.