ningeshauri kuwa serikali iwaajiri waendesha mashitaka ambao kimsingi sio polisi wawe na nguvu yakuendesha mashitaka katika mahakama za mwanzo,hii itasaidia kupunguza mzigo kwa polisi maana wanachunguza wao na wanaprosecute case wao na vile itasaidia kufanya kesi ziwe znatolewa maamuzi haraka pili, raia waelimishwe juu ya haki na sheria zilizopo kuhusu makosa ya jinai why? basically kila binadamu ana haki za msingi ambazo lazima zieshimiwe mfano kwa mshitakiwa ana haki ya kupata dhamana, sasa unakuta mtu kashikwa asubuhi akaweza kujiwekea dhamana jioni akawa mtaani, wananchi wanaanza ooh, polisi wameongwa wamwachie kumbe hapana ni haki ya huyo mshitakiwa.