Polisi yaanza uchunguzi basi la Simba kurudi kinyumenyume, meneja avunja ukimya

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Baada ya kusambaa kwa video ikionyesha basi la timu ya Simba likiendeshwa kinyumenyume, dereva wa basi hilo na meneja wa timu, wamevunja ukimya wa tukio hilo huku jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani likieleza kuendesha gari kinyumenyume umbali mrefu ni kosa.

Jumamosi kabla ya mechi na Raja Casablanca ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Simba ilichapwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, video ya basi hilo likiendeshwa kinyumenyume ilianza kusambaa na kuibua sintofahamu kabla ya dereva aliyejitambulisha kwa jina moja, Peter na Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu kuelezea chanzo cha tukio hilo ambalo polisi, kikosi cha usalama barabarani wamelitolea ufafanuzi.

Kamanda wa Polisi, Kikosi cha Usalama barabarani, Ramadhan Ng'azi alisema kuendesha gari kinyumenyume kwa makusudi ni kukiuka sheria za barabarani.


"Hata hivyo kwa Simba, tutafanya uchunguzi wa tukio hilo kubaini kama lipo au hapana na kama kweli hilo ni basi la klabu hiyo kabla ya kuchukua hatua kwani kipo kifungu kinakataza matumizi mabaya ya barabara kwa kuwa unaweza kuhatarisha maisha ya wengine na vyombo vyao.

"Kwa kufanya hivyo, unaweza kushtakiwa na Mahakama ikikutia hatiani unapigwa faini isiyopungua Sh50,000, hivyo basi kwa tukio la basi linalotajwa ni la Simba, nitaangalia kama lipo au halipo, kwa kufanya uchunguzi kubaini ukweli," amesema.

Mwananchi imezungumza na dereva wa basi hilo ambaye alisema hayuko tayari kuzungumza lolote, lakini atataka meneja wake azungumze kwa niaba yake kwani walikuwa pamoja.

Rweyemamu alisema hiyo si mara ya kwanza kwa basi hilo kuendeshwa hivyo, ingawa video zinazosambaa zimekuzwa kutokana na mechi yao na Raja Casablanca ya Morocco ya hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa.

"Lile ni basi letu ndiyo, na si mara ya kwanza kuendeshwa hivyo japo si kweli kwamba lilitoka Keko hadi Taifa likiendeshwa kinyumenyume," amesema.

Tangu video hiyo kuanza kusambaa, sintofahamu iliibuka baadhi ya watu wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina, jambo ambao Simba wamesisitiza ni uvumi na utani wa jadi tu.

"Ile video pale ni Masaki, kwenye hoteli ambayo timu iliweka kambi (aliitaja) gari haliwezi kugeuza, inabidi lirudi kinyumenyume.

"Dereva ili aweze kupaki vizuri kwani eneo hilo njia ni nyembamba na kuna waya na miti, nyaya za umeme zimeshuka chini, dereva hawezi kugeuza lazima arudi kinyumenyume akageuzie Double tree.

"Wakati video hiyo inachukuliwa hata wachezaji ndani ya basi hawakuwepo, na uendeshaji huo ni kila siku tunapoweka kambi kwenye hoteli hiyo dereva lazima arudishe gari kinyumenyume ili apaki vizuri, lakini kwa kuwa tumefungwa juzi (Jumamosi) ndiyo yamekuzwa hivyo," amesema.

Alisema wanaodai gari limetoka Keko hadi uwanjani (Benjamin Mkapa), si kweli, akihoji kama Keko kuna maghorofa kama yanayoonekana kwenye video ya basi hilo.

"Pale ni Masaki, watu hawajiulizi tu, hivi Keko kuna beach (fukwe), lakini ndiyo hivyo mtu akiamua kusema chochote huwezi kumzuia, ile videoya basi letu ilikuwa ni mchana na pale ni hotelini ambako timu iliweka kambi na basi halikuwa hata na wachezaji, lakini watu wameunganisha na mechi yetu ya juzi (Jumamosi) na kuamua tu kuzungumza," amesema.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clford Ndimbo alisema timu hiyo kwenye mechi na Raja Casablanca iliingia uwanjani na king'ora.

"Sikuona tukio la basi kuendeshwa kinyumenyume, nilichokishuhudia timu iliingia uwanjani kawaida na king'ora kama taratibu za CAF zinavyohitaji, hivyo siwezi kulisemea," amesema Ndimbo.

Ofisa habari wa Simba, Ahmed Ally alisema halifahamu tukio hilo na si kweli kwamba basi la timu yao lilitoka Keko kinyumenyume kama inavyovumishwa.

"Timu iliingia uwanjani kawaida, kabisa tena kwa king'ora, wanaosema basi liliendeshwa kinyumenyume waulizwe vizuri, lakini sikuliona tukio hilo," amesema Ahmed.


Channzo: Mwanachi

Pia soma: Dereva wa basi la Simba matatani kwa kuendesha gari kinyumenyume
 
Mara nyingi tu Basi la Yanga linapita njia ya kinyume na inaachiwa tu.
Yaani inapita barabara inayo yataka magari yaendele kinyume chake.

Mfano magari yetu akienda mbele yanapita kushoto kwa barabara na kutii sheria ya Right hand drive.

Basi la Yanga likiwa na wachezaji wa hiyo timu limepita mara nyingi tu katika njia inayoruhusu left hand drive kiasi cha kuhatariasha usalama wa magari mengine yenye haki ya hiyo njia.
Yaani kama unaenda mbele badala ya kupita kushoto kwa Barabara gali ya Yanga ilikuwa inapita kulia kwa Barabara. Mara nyingi tu nimeona kwa macho yangu.

Anzeni na Yanga Kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…