Polisi yamshikilia Mchungaji EAGT tuhuma za kubaka, kumpa mimba Mwanafunzi

Polisi yamshikilia Mchungaji EAGT tuhuma za kubaka, kumpa mimba Mwanafunzi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1576658794510.png

Polisi wilayani Kisarawe mkoani Pwani, inamshikilia Mchungaji wa kanisa la EAGT la Mtamba, Shauri Steven kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi akimlaghai kupitia huduma ya maombi

Dar es Salaam. Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Mtamba wilayani Kisarawe mkoani Pwani, Shauri Steven anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la tano.

Mwanafunzi huyo amebakwa na kupewa mimba wakati takwimu zikionyesha mwanafunzi mmoja kati ya watatu amekatisha masomo kwa mimba au ndoa za utotoni.

Akizungumza na Mwananchi jana Jumanne Desemba 17, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amesema sababu za mchungaji huyo kubaka na kumpa mwanafunzi mimba ni tamaa za mwili.

Alisema mchungaji huyo alifanikiwa kumlaghai mwanafunzi kwa madai ya kumfanyia huduma ya maombi.

Jokate ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Kisarawe alisema Desemba 12, 2019 mwalimu wa shule ya msingi Mtamba, Justine Mrutu aligundua mwanafunzi huyo mjamzito.

"Alimlaghai kupitia mbinu ya maombi, mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani," alisema Jokate.

Chanzo: Mwananchi
 
Tuhuma kwa viongozi wa kidini ni vyema zikachukuliwa kwa tahadhari ya hali ya juu.
Wakati mwingine ni chuki za kuwaharibia tu.
Hii nimeshuhudia mara kadhaa na wapanga njema meisho huishia kuaibika.
Japo wapo wengi ssna wenye tabia hizi pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusipotokea issues kama hizi hawa viongozi wetu wanaona kama hawafanyi kazi
 
Jokate Mwegelo amesema sababu za mchungaji huyo kubaka na kumpa mwanafunzi mimba ni tamaa za mwili.
 
Tuhuma kwa viongozi wa kidini ni vyema zikachukuliwa kwa tahadhari ya hali ya juu.
Wakati mwingine ni chuki za kuwaharibia tu.
Hii nimeshuhudia mara kadhaa na wapanga njema meisho huishia kuaibika.
Japo wapo wengi ssna wenye tabia hizi pia

Sent using Jamii Forums mobile app

Chuki wapi mkuu na mtoto ana mimba au mimba huyo binti kajipa mwenyewe


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom