Polisi yapiga marufuku magari ya mnadani kubeba abiria

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Siku chache baada ya kutokea ajali iliyoua watu 13 mkoani Ruvuma, Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani, Mossi Ndozero amefanya msako ili kubaini malori yanayopakia abiria na mizigo kwa ajili ya kuwasafirisha kwenda minadani.

Ndozero amepiga marufuku usafiri huo kupakia abiria huku akishusha wafanyabishara waliokuwa wamepanda maroli hayo na kuwataka watafute usafiri mwingine rafiki, ikiwamo kukodi gari.

Kuanzia saa 9 usiku baadhi ya malori hayo yamekuwa yakisafirisha wafanyabishara wanaoenda minadani katika vijiji mbalimbali mkoani Iringa.

Ndozero akiwa na askari wengine wa jeshi hilo, walijitega kwenye barabara ya Iringa- Pawaga na kufanikiwa kubaini maroli hayo ambayo licha ya kupigwa faini, abiria walishushwa na kutakiwa wakodi Coaster.

Kutokana na hali hiyo alipiga marufuku maroli hayo kupakia abiria akiwataka watumie njia nyingine ikiwamo kukodi kosta au haisi, zitakazokuwa zinawapeleka huko.

“Hamjasikia wenzetu wamepoteza maisha huko Ruvuma? Kwanini hilo lisiwe funzo kwenu mpaka tuje kukamatana? Nawaomba sana msitumie malori kusafiri kwenda minadani. Jikusanyeni na mkipakia mizigo basi nyie msafiri na Hiace au Coaster,’ amesema Ndozero na kuongeza;

“Ukiwa kwenye lori na mizigo, likianguka kupona wewe ni jambo gumu, mizigo itakuangukiwa na itakuwa juu yako. Mnapenda kupoteza maisha kizembe?”

Ndozero alikuwa akiwashusha abiria kwenye mabasi hayo kila anapowaona kisha kuwataka watafute usafiri mwingine huku akipiga faini maroli yaliyowapakia.

Akizungumza na wafanyabiashara kwenye minada iliyofanyika katika vijiji vya Ilolo Mpya, jana Aprili 14, 2023, Ndozero aliwataka kutengeneza umoja utakaowasaidia wawe wanakodi magari ya abiria na kuachana usafiri huo.

“Kwa Iringa sitarajii kuona lori lolote linasafirisha abiria, tena mnakaa na kuning’inia juu ya mizigo bila hofua, hii hapana,” amesema Ndozero.

Awali, Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Iringa, Glory Mtui alisema wataendelea kudhibiti mtindo wa magari hayo kupakia abiria.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara walisema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ugumu wa maisha.

“Ni gharama kubwa kusafirisha mizigo na sisi kukodi gari jingine, hali ya uchumi ipo juu na wakati mwingine huko mnadani unaweza kwenda na usiambulie kuuza ndio maana huwa tunaona tujibane kwenye mizigo,” alisema Joseph Ndelwa, mmoja wa wafanyabishara.

Alisema eneo kama Paswaga linayo magari yanayotoka kijiji kila siku asubuhi kuja mjini na kurejea usiku, jambo ambalo ni gumu kwao kuyapanda.

“Mabasi mengi ya vijijini ratiba zao za kusafiri ni ngumu, wanakuja mjini asubuhi na kurudi jioni kiasi kwamba, kwetu ni ngumu kuyatumia hayo,’ amesema.

MWANANCHI
 
Kama kawaida tunaendeshwa na trend.

Kesho utakuta hao hao traffic wanaokamata leo wanachukua hongo kuruhusu usafirishaji huo huo wanaoukataza leo.

Ukute kamanda anamiliki baadhi ya hayo malori. Mbele ya kamera anayapinga nyuma ya kamera anakusanya hesabu yake ya siku.

Nchi ya maigizo.
 
Miaka yote wamekuwa wakitumia malori na mafuso kwenda minadani. Ukizuia mizigo yao itakuwa na usalama kiasi gani?

Hiyo ni ajali tu ambapo hata wakipanda usafiri mwingine inaweza tokea. Ina maana ajali imetokea sababu lori limebeba watu? Basi na mabasi yakipata ajali yasibebe watu.
 
Hawawezi kukubali yaan bora wafe kwa ajali...
Nani atakubali kutanguliza mzgo halafu yeye abaki nyuma
 
Uuuwiii Nina DCM truck langu lipo garage nitalipeleka wapiiii!!?
 
Polisi wa Tanzania wako very reactive. They are never proactive.
Gari la wanafunzi lilipoua wanafunzi kule Mtwara, school bus zote zilitakiwa kukaguliwa.
Juzi juzi baada ya ajali kuongezeka wametangaza kukagua leseni na vyeti. Ndani ya mwezi mmoja magari ya minadani yatakua yanapakia watu Kama kawa.
 
Waliposema gari zisisafiri usiku,wananchi wasomi na wajuvi wa mambo wakasema huo ni ulimbukeni na ni madhara ya kuajiri kidato cha nne.
Hawa watu ndio viumbe wanafanya kazi kwa pressure kubwa sana,kifupi hawana jambo watafanya lionekane ni la maana.

Wangeacha jamii ivune ujinga wake,lakini kuna watoto wasio na chaguo ktk ujinga wa wazazi ama wakubwa wao,wanagharamika sababu ya ujinga wa wakubwa wao.
 
Siku chache baada ya kutokea ajali iliyoua watu 13 mkoani Ruvuma, Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani, Mossi Ndozero amefanya msako ili kubaini malori yanayopakia abiria na mizigo kwa ajili ya kuwasafirisha kwenda minadani.

Ndozero amepiga marufuku usafiri huo kupakia abiria huku akishusha wafanyabishara waliokuwa wamepanda maroli hayo na kuwataka watafute usafiri mwingine rafiki, ikiwamo kukodi gari.

Kuanzia saa 9 usiku baadhi ya malori hayo yamekuwa yakisafirisha wafanyabishara wanaoenda minadani katika vijiji mbalimbali mkoani Iringa.

Ndozero akiwa na askari wengine wa jeshi hilo, walijitega kwenye barabara ya Iringa- Pawaga na kufanikiwa kubaini maroli hayo ambayo licha ya kupigwa faini, abiria walishushwa na kutakiwa wakodi Coaster.

Kutokana na hali hiyo alipiga marufuku maroli hayo kupakia abiria akiwataka watumie njia nyingine ikiwamo kukodi kosta au haisi, zitakazokuwa zinawapeleka huko.

“Hamjasikia wenzetu wamepoteza maisha huko Ruvuma? Kwanini hilo lisiwe funzo kwenu mpaka tuje kukamatana? Nawaomba sana msitumie malori kusafiri kwenda minadani. Jikusanyeni na mkipakia mizigo basi nyie msafiri na Hiace au Coaster,’ amesema Ndozero na kuongeza;

“Ukiwa kwenye lori na mizigo, likianguka kupona wewe ni jambo gumu, mizigo itakuangukiwa na itakuwa juu yako. Mnapenda kupoteza maisha kizembe?”

Ndozero alikuwa akiwashusha abiria kwenye mabasi hayo kila anapowaona kisha kuwataka watafute usafiri mwingine huku akipiga faini maroli yaliyowapakia.

Akizungumza na wafanyabiashara kwenye minada iliyofanyika katika vijiji vya Ilolo Mpya, jana Aprili 14, 2023, Ndozero aliwataka kutengeneza umoja utakaowasaidia wawe wanakodi magari ya abiria na kuachana usafiri huo.

“Kwa Iringa sitarajii kuona lori lolote linasafirisha abiria, tena mnakaa na kuning’inia juu ya mizigo bila hofua, hii hapana,” amesema Ndozero.

Awali, Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Iringa, Glory Mtui alisema wataendelea kudhibiti mtindo wa magari hayo kupakia abiria.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara walisema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ugumu wa maisha.

“Ni gharama kubwa kusafirisha mizigo na sisi kukodi gari jingine, hali ya uchumi ipo juu na wakati mwingine huko mnadani unaweza kwenda na usiambulie kuuza ndio maana huwa tunaona tujibane kwenye mizigo,” alisema Joseph Ndelwa, mmoja wa wafanyabishara.

Alisema eneo kama Paswaga linayo magari yanayotoka kijiji kila siku asubuhi kuja mjini na kurejea usiku, jambo ambalo ni gumu kwao kuyapanda.

“Mabasi mengi ya vijijini ratiba zao za kusafiri ni ngumu, wanakuja mjini asubuhi na kurudi jioni kiasi kwamba, kwetu ni ngumu kuyatumia hayo,’ amesema.

MWANANCHI
Polisi waongo tangu wameaza kutoa makatazo hayo sio leo zaidi wana watengenezea alaji polisi barabalani mwezi ulio pita IT iliuwa watu mikumi polisi wakatoa tamko la kupiga marufuku magali hayo kukeba abiria siku ya j 4 nenda pale kimala mbezi Morogoro msavu Dodoma hivi ni vituo vio via kubeba abiria waendao kanda ya ziwa polisi waongo wanajikosha tu hawana uwezo huo
 
Back
Top Bottom