BREAKING NEWS : Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema msaidizi wa @BenMembe Jerome Luanda yuko mikononi mwa polisi na ni mzima wa afya hivyo wanaodai ametekwa ni waongo.
====
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, leo Septemba 17, 2020, amesema msaidizi wa Mgomba Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe, aitwaye Jerome Luanda, yuko mikononi mwa polisi akiwa ni mzima wa afya na hakutekwa.
Amesema hayo akiwa anazungumza na East African Radio ya jijini Dar es Saalam, ambapo amethibitisha msaidizi huyo alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na akakanusha habari za kutekwa.
“Huo ni uongo na uzushi; tumemkamata akiwa airport pale Julius Nyerere, nasikia wengine wanasema wamemtafuta vituo vyote hawajamuona. Ni uongo, sisi tupo naye na ni mzima wa afya, tunamshikilia kutokana na kesi zake ambazo hatuwezi kuzitaja,” amesema na kuongeza:
“Na huyu nasema amekamatwa, anatuhumiwa kwa kosa la kutakatisha fedha, kwa hiyo anayetaka kuthibitisha hilo ni suala la kuja tumueleze ukweli wa jambo hilo.”
Tukio hilo limejiri baada ya Mgombea Urais huyo, kuandika katika ukurasa wake wa Twitter Septemba 16, 2020, kuwa msaidizi wake amechukuliwa na watu wasiojulikana, na hivyo akatoa masaa kadhaa ili awe amepatikana.
BREAKING NEWS : Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema msaidizi wa @BenMembe Jerome Luanda yuko mikononi mwa polisi na ni mzima wa afya hivyo wanaodai ametekwa ni waongo...
Mwambieni mambo sasa baada ya Tar 28/10 faili zote hapo ofisini kwake ziwe na taarifa sahihi- akumbuke ofisi yoyote ya serikali inasimamiwa kwa mujibu wa sheria, kama anafanya mambo kinyume na utaratibu basi huko anakoshikilia watu asishangae na yeye akashikiliwa huko
BREAKING NEWS : Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema msaidizi wa @BenMembe Jerome Luanda yuko mikononi mwa polisi na ni mzima wa afya hivyo wanaodai ametekwa ni waongo...
Hili likamanda ni litekaji litesaji limeshiriki uhalifu mwingi sana! Linamchukuaje mtu bila taarifa kutolewa? Mwanausalama wa hovyo kwenye mfumo wa hovyo hovyo!
Labda tumkumbushe Mambosasa kuwa taratibu za kisheria za polisi kumkamata mhalifu zipo wazi, sasa iweje wewe umemvizia na kumkamata bila kujitambulisha wala kuwataarifu ndugu zake? Sasa umejidhihirisha kuwa wewe ni mtekaji na muuaji! Bila kutishiwa ungekaa kimya na huenda tungeokota maiti!
Duuh kwani angemfanyaje zaidi labda ya kulalamika tu kwenye media maana huwa najaribu kuimagine mikwara mama hiyo utekelezaji wake unakuwaje nashindwa kuelewa.
Duuh kwani angemfanyaje zaidi labda ya kulalamika tu kwenye media maana huwa najaribu kuimagine mikwara mama hiyo utekelezaji wake unakuwaje nashindwa kuelewa.