Pre GE2025 Polisi yatoa taarifa ya kukamatwa kwa viongozi na wafuasi wa CHADEMA, wawataka kufuata sheria

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
TAARIFA KWA UMMA
12 Agosti, 2024
Jeshi la Polisi linapenda kutoa taarifa kwa umma kufuatia katazo na kupiga marufuku kongamano la vijana wa CHADEMA lililokuwa limepangwa kufanyika katika uwanja wa Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya siku ya jumatatu Agosti 12, 2024 kwa mwamvuli wa kuadhimisha siku ya vijana duniani.

Kufuatia katazo hilo, kwa siku ya jana Agosti 11, 2024 Jeshi la Polisi liliwakamata viongozi na wafuasi wa CHADEMA 375 kati yao wanaume 261 na wanawake 114, ambao walikaidi na kuendelea kufanya safari kutoka mikoa mingine kwa lengo la kutaka kuingia Mkoa wa Mbeya kupitia njia mbalimbali ili kutimiza azma hiyo ovu ya kufanya kongamano lililopigwa marufuku. Waliokamatwa wakiwa njiani kwenda Mkoa wa Mbeya na kukamatiwa Mkoa wa Morogoro walikuwa 28, Mkoa wa Iringa walikuwa 109, Mkoa wa Njombe walikuwa 60, Mkoa wa Dar es Salaam walikuwa 19, Mkoa wa Pwani walikuwa 41, Mkoa wa Rukwa walikuwa 30 na Mkoa wa Songwe walikuwa 51.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa

Kati ya watuhumiwa waliokamatwa walikuwemo viongozi wakuu wa CHADEMA waliokamatiwa Mkoa wa Mbeya eneo la Kadege ambao ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu, Katibu Mkuu, John Mnyika, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi @ Sugu, Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa, Twaha Mwaipaya na Makamu Mwenyekiti BAVICHA Taifa, Moza Ally.

Agosti 12, 2024 Jeshi la Polisi liliwakamata wafuasi wengine wa CHADEMA 145 kati yao wanaume 112 na wanawake 33 wakiwemo viongozi wakuu wa chama hicho, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA), John Pambalu, ambao walikamatwa uwanja wa ndege wa Songwe wakiwa tayari wamekwishafika

Mkoani Mbeya kwa ajili ya kushiriki kwenye kongamano ambalo lilipigwa marufuku. Hivyo, jumla ya watuhumiwa wote waliokamatwa ni 520 na magari 25.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akamatwa uwanja wa Ndege Songwe

Aidha, jumla ya magari 20 aina ya Toyota Coaster yalikamatwa kutoka maeneo mengine kwenda Mkoa wa Mbeya ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam yalikamatwa magari matatu (3), Pwani magari matatu (3), Morogoro magari matatu (3), Iringa magari matatu (3), Njombe magari matatu (3), Songwe magari matatu (3) na Rukwa magari mawili (2). Watuhumiwa waliokamatwa walibainika kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Simiyu, Dodoma, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Mara na Zanzibar.

Watuhumiwa wote walihojiwa kisha kurejeshwa maeneo walikotoka kwa kusindikizwa na Polisi (Police escort).

Kwa Mkoa wa Mbeya, jumla ya magari matano (5) ambapo Mitsubishi Canter 2, Toyota Coaster 2 na Mitsubishi Fuso 1 yalikamatwa yakitokea Wilaya ya Mbeya, Chunya na Kyela. Watuhumiwa waliokamatwa Mkoa wa Mbeya, wamehojiwa na kupewa dhamana na wengine ambao ni viongozi wa CHADEMA wamerudishwa walikotoka kwa kusindikizwa na Polisi (Police escort)

Pia soma: Uzi Maalum wa Matukio ya Kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Jeshi la Polisi linaendelea kuimarisha ulinzi katika Jiji la Mbeya na Mikoa yote Tanzania ambako wanategemea kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani ili visifanyike. Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali zinazopangwa kuhusiana na mipango ya kufanya

uvunjifu wa amani na yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria bila kujali cheo, wadhifa au itikadi yake.

Jeshi la Polisi linawataka viongozi wa vyama vya siasa na wafuasi wake kufuata sheria na taratibu za nchi na kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu au kikundi cha watu watakaojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani. Mwisho tunaendelea kuwaomba wananchi kutii sheria bila shuruti.

Imetolewa na:
Awadh J. Haji - CP
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo,
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania.

IMG_20240813_071542_488.jpg
IMG_20240813_071542_170.jpg
 
TAARIFA KWA UMMA
12 Agosti, 2024
Jeshi la Polisi linapenda kutoa taarifa kwa umma kufuatia katazo na kupiga marufuku kongamano la vijana wa CHADEMA lililokuwa limepangwa kufanyika katika uwanja wa Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya siku ya jumatatu Agosti 12, 2024 kwa mwamvuli wa kuadhimisha siku ya vijana duniani.

Kufuatia katazo hilo, kwa siku ya jana Agosti 11, 2024 Jeshi la Polisi liliwakamata viongozi na wafuasi wa CHADEMA 375 kati yao wanaume 261 na wanawake 114, ambao walikaidi na kuendelea kufanya safari kutoka mikoa mingine kwa lengo la kutaka kuingia Mkoa wa Mbeya kupitia njia mbalimbali ili kutimiza azma hiyo ovu ya kufanya kongamano lililopigwa marufuku. Waliokamatwa wakiwa njiani kwenda Mkoa wa Mbeya na kukamatiwa Mkoa wa Morogoro walikuwa 28, Mkoa wa Iringa walikuwa 109, Mkoa wa Njombe walikuwa 60, Mkoa wa Dar es Salaam walikuwa 19, Mkoa wa Pwani walikuwa 41, Mkoa wa Rukwa walikuwa 30 na Mkoa wa Songwe walikuwa 51.

Kati ya watuhumiwa waliokamatwa walikuwemo viongozi wakuu wa CHADEMA waliokamatiwa Mkoa wa Mbeya eneo la Kadege ambao ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu, Katibu Mkuu, John Mnyika, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi @ Sugu, Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa, Twaha Mwaipaya na Makamu Mwenyekiti BAVICHA Taifa, Moza Ally.

Agosti 12, 2024 Jeshi la Polisi liliwakamata wafuasi wengine wa CHADEMA 145 kati yao wanaume 112 na wanawake 33 wakiwemo viongozi wakuu wa chama hicho, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA), John Pambalu, ambao walikamatwa uwanja wa ndege wa Songwe wakiwa tayari wamekwishafika

Mkoani Mbeya kwa ajili ya kushiriki kwenye kongamano ambalo lilipigwa marufuku. Hivyo, jumla ya watuhumiwa wote waliokamatwa ni 520 na magari 25.

Aidha, jumla ya magari 20 aina ya Toyota Coaster yalikamatwa kutoka maeneo mengine kwenda Mkoa wa Mbeya ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam yalikamatwa magari matatu (3), Pwani magari matatu (3), Morogoro magari matatu (3), Iringa magari matatu (3), Njombe magari matatu (3), Songwe magari matatu (3) na Rukwa magari mawili (2). Watuhumiwa waliokamatwa walibainika kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Simiyu, Dodoma, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Mara na Zanzibar.

Watuhumiwa wote walihojiwa kisha kurejeshwa maeneo walikotoka kwa kusindikizwa na Polisi (Police escort)
Kwa Mkoa wa Mbeya, jumla ya magari matano (5) ambapo Mitsubishi Canter 2, Toyota Coaster 2 na Mitsubishi Fuso 1 yalikamatwa yakitokea Wilaya ya Mbeya, Chunya na Kyela. Watuhumiwa waliokamatwa Mkoa wa Mbeya, wamehojiwa na kupewa dhamana na wengine ambao ni viongozi wa CHADEMA wamerudishwa walikotoka kwa kusindikizwa na Polisi (Police escort)

Jeshi la Polisi linaendelea kuimarisha ulinzi katika Jiji la Mbeya na Mikoa yote Tanzania ambako wanategemea kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani ili visifanyike. Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali zinazopangwa kuhusiana na mipango ya kufanya

uvunjifu wa amani na yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria bila kujali cheo, wadhifa au itikadi yake.

Jeshi la Polisi linawataka viongozi wa vyama vya siasa na wafuasi wake kufuata sheria na taratibu za nchi na kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu au kikundi cha watu watakaojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani. Mwisho tunaendelea kuwaomba wananchi kutii sheria bila shuruti.

Imetolewa na:
Awadh J. Haji - CP
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo,
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania.

View attachment 3068357View attachment 3068358
Grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr !!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom