Pre GE2025 Polisi yazuia CHADEMA kufanya mikutano Tarafa ya Ngorongoro kutokana na sababu za Kiintelejensia!

Pre GE2025 Polisi yazuia CHADEMA kufanya mikutano Tarafa ya Ngorongoro kutokana na sababu za Kiintelejensia!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Jeshi la Polisi limesema taarifa za kiintelejensia zinaonesha Tarafa ya Ngorongoro si salama sana Kwa sasa hivyo Chadema hawataruhusiwa kufanya mkutano kwenye Operesheni yao itakayoanza kesho

Chadema wameafiki na kufuta mikutano ya Tarafa ya Ngorongoro
---
Siku moja kabla ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuanza operesheni ya kukijenga chama hicho Kanda ya Kaskazini, chama hicho kimesema hakitafika kwenye Tarafa ya Ngorongoro.

Uamuzi huo unafuatia zuio la Polisi Wilaya ya Ngorongoro la Juni 20, 2024 kuwa taarifa za kiintelijensia zinaonyesha eneo la tarafa hiyo si salama kwa sasa kufanyia shughuli za kisiasa.

Chadema inatarajia kufanya operesheni ya siku 21, kuanzia kesho Juni 22, 2024 kwenye majimbo 35 ya mikoa ya Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro, ikiongozwa na mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Juni 21, 2024, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa amesema baada ya uongozi wa wilaya kupokea barua hiyo, wameshauriana na kuamua kuridhia suala hilo.

Amesema kutokana na sababu hiyo, mikutano iliyokuwa ifanyike katika Ngorongoro, itafanyika tarafa za Sale na Loliondo, ambazo pia zipo wilayani humo.

Source: Mwananchi
 
Hao wamasai wa Ngorongoro lazima watakwenda kusikiliza hoja za ukombozi za Chadema katika tarafa za jirani.
 
Back
Top Bottom