figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Heshima kwenu wakuu,
Kigugumizi cha nini baba?
Padri wa Kanisa Katoliki, Evaristus Mushi aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akiegesha gari kando na Kanisa la Mtoni mwaka 2013, rais Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi, aliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya ndani na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alihusisha tukio hilo na vitendo vya ugaidi wakati akitoa tamko la Serikali na kueleza kuwa Rais Kikwete ameidhinisha Serikali kugharamia wapelelezi kutoka nje kufanyia kazi swala hilo.
Serikali ya Marekani iliyokuwa tayari kusaidia upelelezi wa mauaji hayo, ambapo haraka sana ASKARI wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), waliwasili Zanzibar kufanya uchunguzi wa kuwabaini waliomuua kwa kumpiga risasi, Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki.
Napenda kujua kwanini awamu hii ya tano wanakuwa na kigugumizi kuwashughulikia watu wasiojulikana?
Hii ilikuwa mara ya pili kwa FBI kuja nchini kufanya operesheni kubwa ya upelelezi. Mwaka 1998 walifika kuchunguza kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani na kugundua kuwa Kundi la Al-Qaeda lilihusika.
Aidha hiyo ni mara ya tatu kwa wapelelezi wa Tanzania kushirikiana na wageni kuchunguza matukio ya uhalifu baada ya mwaka 1984, Idara ya Upelelezi ya Uingereza, Scotland Yard ya Uingereza kuchunguza kuungua kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Watu wasiojulikana wanaenda kuiweka Tanzania roho juu. Kwanini Mwigulu hachukui hatua aliyoichukua mwenzake Nchimbi 2013?
Baada ya FBI kufanya uchunguzi Zanzibar, ilitoa picha ya mchoro ya mtu anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi Padre Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki.
Mchoro huo ulisambazwa katika vyombo vya habari kutoka ofisi ya Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa na ulimuonesha ‘mtu’ aliyevaa baraghashia….
Tunaomba Serikali ya Magufuli itusaidie kutupatia japo mchoro tu wa watu wasiojulikana.
Jisomee=>Muuaji wa Padri Evarist Mushi Akamatwa kwa msaada wa picha iliyochorwa na FBI
FBI waondoka Zanzibar bila polisi kujua
PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana
~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana