Pombe Imenivua Nguo, Nimemtamkia Bibi Harusi Matusi ya Nguoni kwenye Nasaha

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2017
Posts
6,097
Reaction score
7,199
Wanajukwaa,

Nashea na nyie jinsi mseto wa pombe ulivoniaibisha nikatukana siku nilipoitwa kutoa nasaha kwa niaba ya baba wa bibi harusi kwakua mzazi wake anakigugumizi asingeweza kuendana na kasi lakn pia wageni wasingemuelewa.

Ilikua mwaka 2016 mwezi Mei Nzega nilihudhuria harusi ya mtoto wa Binamu yangu, kama kawaida nilipania sana pombe. Siku ile nilikunywa sana Balimi nikamix na mzinga wa K-Vant. Nilikua na wananzengo tu wife ye hakuja harusini.

Mara paa, akaja shangazi yake na baba wa bwn harusi akaniomba nikatoe nasaha kwa niaba ya mzazi wa bibi harusi kwakua babake hua anakigugumizi sugu. Sikujietathmin hata kama ntaweza ile kaz au la, nikaendelea kula bia nikijua ntapambana na hali yangu, labda tena ntakua na konfidensi zaidi kutokana na nilivochapa mtungi.

Skumbuki ilikuaje wakat wa nasaha, ila nilisikitika kuambiwa kwamba nilimuasa bibi harusi kwa ukali sana na nilitumia maneno makali kupitiliza. Naambiwa nilitamka visivyotamkwa na nilirudia mara kwa mara maneno "https://jamii.app/JFUserGuide you".

Naambiwa kwamba bibi harusi alifedheheka sana na alikua akilia wakat waalikwa wengine walikua wanaangua kicheko na kwakua nilikua nataka sifa kwaajili ya pombe, nilikua hata simuangalii bi harusi, niliwageukiwa wageni waalikwa na kutoa maneno ya kuudhi sana. Kwenye ile ya CD ya harusi nimeambiwa wamekata hotuba yangu japo kipande kilichopo najiona nikiwa nimekunja ndita na kuongea kwa ukali huku mate yaliyogeuka mapovu meupe yamenijaa.

Nilijutia na kuomba msamaha kwenye kikao cha ukoo. Walinisamehe wengine kwa shingo upande

Balimi mixer K-Vant
 
Inashangaza mzazi au mlezi badala ya kupongeza/kuwatakia mema maharusi, inakuwa ndio nafasi ya kuwaonya kama vile hawajui nini matokeo/ majukumu ya uamuzi wao.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka kwa nguvu balimi haijawai mwacha mtu salama halafu mixer kvant pole
 
Pole mlevi mwenzangu. Mimi nilishawahi kujitapikia watu wamenisafisha vizuri asubuhi nikaanza kulalamika kwa sauti nani katapika humu na matusi juu...
Dah harusi hizi! Hapo pia K Vant ilihusika...
 
Ila kwa kuwa ulitukana kizungu,sio wewe,pombe ndio ilitukana,wewe uko safi kama sufu
 
Kama hii story siyo ya ya kutunga, Basi wahusika na waalikwa wa Sherehe hiyo wote walikuwa wajinga kupitiliza.

Inapotokea tukio la aina hiyo, basi muhusika ahairishiwe na kutolewa mahali hapo ama DJ akatishe kwa kuendelea na ratiba nyingine.
Tena mtoa nasaha hapaswi awe amegusa kilevi chochote kabla ya utaratibu mzima......
 
Siku nyingine jaribu kujicontrol,, maana utajikuta umepasuliwa mayai mtaroni kisa pombe za kijinga
 
Dah...inaonekana kama wote walilewa[emoji87]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…