Pombe inaharibu maisha yangu nisaidieni

Mkuu pole sana...Tafuta kitabu kinaitwa "ATOMIC HABITS- by James Clear"....Kitakusaidia sana kama kweli upo tayari kubadilika. It's one of the best books when it comes to habits....

Mimi kilinisaidia sana, sana.
 
Pole mkuu.

Roho ya ulevi hiyo inakutesa.

Rabbon
 
Mkuu ACHA kabisa nimeona familia zikisambaratika KISA pombe mkuu
 
Achana na marafiki wapenda pombe, usipange sehemu ambayo ipo karibu na bar na mwisho ni muda Sasa wa kumtumikia Mungu maana muda wa kwenda bar utakuwa ibadani
 
Nenda ujisalimishe kwenye nyumba za kuwakarabati walevi, siku hizi zipo nyingi achana na maombi kwanza.
 
Pole sana Mkuu.. Jiungamanishe kwenye maombi kuikataa hiyo roho.. Na uchawi huwa hautoki mbali, hukohuko kwenye hayo mabaa ndo wamejaa wachawi ambao huwa wanawafunga walevi waendelee kulewa, wawe walevi zaidi na kutumia hela nyingi. Na hao malaya pia wengi wao wameunganishwa na madhabahu za kuzimu ambazo zinaendelea kukushikilia kwenye hiyo cycle... Suluhu ni Nguvu ya Mungu iingilie kati.
 
Bora pombe sio betting
 
hao madada wa kisambaa hawajakuacha lazima upigwe juju! usiechezee chezee mabint wa watu huko! huko kila nyumba kuna mganga sasa utapona kweli kurogwa?
 
Mwambie Yesu, ongea nae kama mzazi wako. Muelekezee tatizo lako kama ulivyotueleza hapa. Mwambie hata ukiwa umelewa hapo.
 
Tukusaidie kwa kukunyang'anya glass au?
 
Kwa hali uliyofikia wewe mwenyewe huwezi kuacha; utaacha kwa sababu huna hela, ila ukipata hela lazima urudi kule kule kwenye pombe.
Wapo wanaoweza kuacha pombe kwa ridhaa yao wenyewe, kama hilo tatizo halina mahusiano na maagano
Ila kama kuna maagano, hutoacha, mpaka upate mtu wa kukushika mkono.​
 
Zaidi ya pombe, je una starehe gani nyingine ambayo kwa mfano ukiacha pombe ndio utakua unaifanya?
 
Kwanza pole Sana lakini pia hongera kwa kutambua kwamba pombe kwako ni tatizo, hiyo ni hatua ya Kwanza.
Mabadiliko ya mtu yeyote huanza na yeye mwenyewe, Utu wako wa ndani una nguvu kubwa kushinda utu wako ya nje kwasababu siku zote nguvu ya nje hujipambanua kwasababu Ile ya ndani imekubali iwe hivyo lakini nguvu ya ndani akikataa nguvu ya nje haiwezi kujipambanua.
Addition!
Nuia kwamba hutaki kunywa pombe. Hapa unaweza kuchukua peni na notebook andika kwa maandishi kwamba hutaki pombe ukimaliza kuandika chini Yake andika Mungu nisaidie.
Jitahidi Kila siku usiku Sana Amka na usali( kusali si lazima upayuke au ujue Sana) maneno machache Tu na usome pale ulipoandika kwamba hutaki pombe malizia lile neno Mungu nisaidie, hata kama Una pombe kichwani do it kwa Imani yako.
Kila la heri mkuu,ila bado nasisitiza ukiamua kwa Ile nguvu yako ya ndani kuacha pombe utaacha
 
pole sana kaka,hiyo ni ROHO CHAFU ya kuzimu inayokufunga katika kifungo cha kutumikishwa na shetani kuwa CHINI ya kifungo cha ulevi,umaskini,magonjwa,mafarakano,uzinzi,uchafu,ajali,fedheha/aibu,kuondolewa kibali,kuvikwa vazi la aibu ,roho ya kukataliwa,na mwisho wa siku ni mateso,uharibufu mkubwa na hatimaye MAUTI.

HATUA ZA KUFUATA ILI KUACHA POMBE
1.Ni kutambua kuwa pombe ni TATIZO na kutambua kuwa pombe ni adui yako,pombe inakuletea uharibifu kuliko faida ambayo haipo ..KISAYANSI pombe imethibitika ina madhara kiafya kwa kiwango chochote hata tone moja,hakuna kiwango chochote hata kiwe kidogo kiasi gani ambacho kina faida kiafya mwilini hata iwe wine hata iwe tone moja.WHO no amaount of alcohol is safe to drink(KIMWILI)

KIROHO pombe na ulevi ni dhambi.na mshahara wa dhambi mauti..pia ukiwa mlevi unafungilia mlango wa roho nyingine chafu za giza kukushambulia,ndio maana ulevi huambatana na uzinzi,kamari,ugomvi,uvutaji sigara ,uongo,uvivu,N.K

2.Hatua ya pili ni KUTAMKA kwa kuungama mbele ya Mungu wewe ja Mungu wako,tubu dhambi ya ulevi ongea na Mungu wako,omba msaada,lakini pia ongea na roho chafu hiyo IKEMEE iambie wewe roho mchafu wa ulevi na baba yako shetani nimeshagundua nyie ndio mnanitesa,SASA nawatangazia kwa jina la YESU sitakuwa chini ya kifungo cheni,sasa niko huru nimeokolewa na Yesu,nakataa kutumikishwa na roho chafu,nataka niishi chini ya mpango na kusudi la Mungu aliyeniumba niyaishi mapenzi ya Mungu,toka shetani,maandiko yanasema mpingeni shetani naye atawakimbia
yanasema zaidi..YESU alituokoa katika nguvu za giza akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake.

3)IMANI amini kuwa inawezekana kuishi bila kunywa pombe ,amini inawezekana kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na jamii yako,amini Mungu anakupenda na anakuwazia mema na anaapenda uishi maisha yanayompendeza,amini Mungu yupo pamoja nawe,amini umekwisha acha pombe.Amini wanaishi bila kunywa pombe sio wajinga/sio washamba.

4)Badilisha ratiba ile ratiba ya kwenda kwenye vilabu vya pombe fanya jambo lingine jema na halali,epuka kuwa maeneo yenye vilevi kama sio lazima.Na kama ukiwa maeneo yenye vilevi kama ni lazima kuwepo hapo kunywa kinywaji kingine kisicho na kilevi.
Kataa mialiko ya kunywa pombe.

5)PESA hasa siku za mwanzo jaribu kumpa pesa mkeo akutunzie ,akupe nauli tu na pesa ndogo ya kutumia EPUKA kutembea na pesa mfukoni.Mpaka utakapozoea

6)IBADA anza kusali na kuhudhuria ibada na semina za neno la Mungu ule muda uliokuwa unaenda kunywa pombe unaweza kuutumia kwa ibada,siku hizi kuna video youtube za mahubiri promover tv..mchungaji AMIEL KATEKELA..ana mahubiri mazuri sana ,ila angalia usitumbukie kwa manabii wa uongo hawa wa vitu vya upako..ni bora usali mwenyewe kuliko kwenda kwenye hawa manabii wa uongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…