[SUP]25[/SUP]Usijioneshe kuwa hodari wa kunywa kileo,
yaani, mvinyo imewaangamiza wengi.
[SUP]26[/SUP]Tanuru hujaribu kazi ya mhunzi,
na mvinyo mioyo ya watu,
katika ugomvi na wenye viburi.
[SUP]27[/SUP]kwa wanadamu mvinyo ni ama maji ya uzima,
ukinywa kwa kiasi.
Je, anao uzima gani mtu asiye na mvinyo?
Nayo imeumbwa ili kuwafurahisha wanadamu.
[SUP]28[/SUP]Mvinyo ni furaha ya moyo na changamko ya roho,
ikinywewa kwa wakati wake na ya kutosha.
[SUP]29[/SUP]Lakini kunywa mno ni uchungu wa roho,
na fedheha na ugomvi.
[SUP]30[/SUP]Kileo humzidishia mpumbavu mitego ya kumletea hasara;
hupunguza nguvu, na zaidi huleta jeraha.
[SUP]31[/SUP]Usimkaripie jirani yako penye karamu ya mvinyo,
wala usimdhihaki anapocheka;
wala usimwambie neno la shutuma,
wala usimnyeye kwa kutaka alipe deni.
Yoshua Bin Sira 31:25-31