Pombe miongoni mwa vichocheo vya ngono zembe

Pombe miongoni mwa vichocheo vya ngono zembe

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Jambo hili nililiona kwa ndugu, rafiki na mwanafunzi mwenzangu tukiwa masomoni huko chuo kikuu. wakati huo nilikua mshirika wa unywaji kabla ya kuamua bila shuruti kuachana na hiyo habari kwa hiyari bila shuruti. haikua na shida kwangu ila sikuona umuhimu wake nikaacha...

Tukiwa masomoni, darasani au mapumzikoni hostel haikua shida. swala la mapenzi au ngono hailikua kipaumbele, wala hapakua na ratiba, stori za mapenzi au mipango ya mapenzi na marafiki wa kike.

shida ilikua kila tukienda kula gambe sasa, rariki yangu akishapakia gambe zake kadhaa tu, kurudi hostel ndio basi tena nitolee hiyo. Ni lazima aopoe muhudumu akalale nae. Na alipendelea zaidi mameneja wa hizo bar au clubs. Ikiwa sio meneja basi lazima iwe muhudumu na sio mteja mwenzie.

sasa imenishangaza katika ajira yangu ya kwanza kwenye taasisi flani ya fedha nikakutana na rafiki wa tabia hiyo. Huyu sasa afadhalli tukiwa wote anaweza kunusurika walau kuporwa cm au computer, ila akiwa mwenyewe akiopoa nae lazima aopolewe kila kitu hususan fedha, simu, sasa ya mkononi, cheni, computer na wakati mwingine viatu vikali alivyovaa.

Lakini akisha piga gambe la kutosha na ameshiba vizur, harudi tena nyumbani, na lazima aopoe na akalale na pisi kali mpaka kukuche.

kwenye ajira ya pili na hii ya sasaivi I have mate the same character friends na kuna moja mpaka ana pigwa makonzi na makofi na mkewe but ataacha two, three week anarudi kwenye uraibu huo wa pombe na ngono kitu ambacho kinahatarisha afya zao binafsi, wenza na ndoa zao.

sasa najiuliza wale wote wanao jaa kwenye bar na clubs wakinywa pombe hitimisho la starehe zao huishia kwenye ngono?

kama ni hivyo, au labda nawe ni miongoni mwa wenye tabia kama za hawa rafiki zangu, ambao hivi sasa wana familia zao. Ni hatari sana, achana tu na pombe au kunywa kiasi kistaarabu 🐒

na halafu kwa wanawake nayo pombe inawachochea kwenye hitimisho la kufanya ngono kama hao rafiki zangu wakiume?

ijulikane bayana, sikatazi au kumzuia yeyote asinywe pombe nashauri tu kunywa kistaarabu 🐒

vichocheo vinginevyo ni kama vile hali ya hewa, hususani baridi...
 
Huo ni ukweli kwa asilimia mia ,pombe huleta maumivu ya nafsi kesho yake baada ya kugundua aidha mwenyewe au kuelezwa ulichofanya jana ,hili huishi kumtafuna mhusika kwa asilimia zote na pengine kwa uchache kuwaahidi watu walio katika circle yake kua hatorudia.
Maamuz mengi yanayofanywa na mnywaji akiwa amewaka huleta majuto makuu kesho yake,ila ni ngumu kuliweka wazi hili.

Mara elfu moja ya mvuta bangi smart mnaweza kupanga mipango ila sio pombe , ni mhanga mmoja wapo ila najitahidi sana kuitua hii kitu na iwe hivo
 
Sio kweli Kuwa pombe ni chanzo cha ngono zembe

Sema kichwa cha chini kikianza kufikiri bila kushirikisha kichwa cha juu kinaweza kufanya jambo lolote hata kichaa unaparamia..

Baadaye sasa ,unaanza ayaa hivi ni mimi kweli?
nara nyingi hiyo ya kufanya lolote mfano hata kufanya mapenzi hata na mtu asie timamu, ni kichocheo cha mazingira, mathalani gizani unahisi hakuna anae kuona na mazingira yanakuchochea kutenda utakachojutia baadae...

why rafiki zangu hawakuwahi kuchukua uamuzi wa kuchukua pisi kali wakiwa hawajatumia hiyo kitu?

ila wakitumia tu lazima wachomoke na pisi kali :BASED:
 
Huo ni ukweli kwa asilimia mia ,pombe huleta maumivu ya nafsi kesho yake baada ya kugundua aidha mwenyewe au kuelezwa ulichofanya jana ,hili huishi kumtafuna mhusika kwa asilimia zote na pengine kwa uchache kuwaahidi watu walio katika circle yake kua hatorudia.
Maamuz mengi yanayofanywa na mnywaji akiwa amewaka huleta majuto makuu kesho yake,ila ni ngumu kuliweka wazi hili.

Mara elfu moja ya mvuta bangi smart mnaweza kupanga mipango ila sio pombe , ni mhanga mmoja wapo ila najitahidi sana kuitua hii kitu na iwe hivo
:KasugaYeah: pole pole ndio mpango, kila la kheri
 
Back
Top Bottom