Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
Inabidi na huyu mwanaume ampokee bwana ni kweli harufu ya pombe na sigara ni kero kama wewe si mtumiaji
Huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kuna rafiki yangu kaniambia kuwa mkewe amemuomba watengane vitanda kwa kuwa mama hataki harufu ya pombe na sigara. Rafiki yangu hataki kufanya hivyo kwa kudai ndoa ni kuvumiliana; na zaidi kuwa walipooana miaka 10 iliyopita pombe na sigara halikuwa tatizo; isipokuwa kuanzia mwaka jana ambapo mkewe alimpokea Bwana Yesu na kuyaacha ya kale. Rafiki yangu anasema yuko tayari kuoa mwanamke mwingine badala ya kuacha mazoea yake au kulala vitanda viwili wakiwa wanandoa.
Mnawashaurije wanandoa hawa?