Kitu ambacho si kielewi ni hiki, watu wengi wanalalamika Zanzibar imeshamiri kwa pombe, umalaya na sigara, tufanye ni kweli. Serikali imeamua kuchukua hatua na kuja na sheria watu bado wanalalamika tena.
Nnachojiuliza, wachangiaji wanatetea hivyo vitu vilivyopigwa marufuku au wanaibeza serikali kwa kuamua kuchukua hatua kupambana na haya majanga?
Nadhani tungeunga mkono juhudi za serikali za kuonyesha nia ya kukerwa na haya mambo kisha tupendekeze njia bora zaidi zinazostahili kuchukuliwa kama tunaona hii ya sasa haitaleta mafanikio.
Kwa uwajibikaji na kuchukua hatua, serikali ya mapinduzi wako vizuriganisha na bara, mfano:-
Tume zilizoundwa kuchunguza ajali za meli na boti zote zilishamaliza kazi, zikatoa mapendekezo yake na hatua zimeshachukuliwa. Tofauti na bara ambako hadi leo uwajibikaji wa tume mbalimbali bado unalalamikiwa na wengi.
Pili, wameweza kudhibiti matumizi na uingizwaji wa mifuko ya nailon, vita hii hata bara iko, lakini hijafanikiwa kabisa.