kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Taasisi ya kimataifa ya uwiano
wa uzito na lishe ya Slimming
World yenye makao yake
makuu nchini Uingereza,
imefanya uchunguzi kuhusu
watu wanaokunywa pombe na kubaini kuwa inawaongezea
kasi ya kula kupita kiasi ndani
ya saa 24. Wakitumia utafiti wa moja
kwa moja wa kuwahusisha
wanywa pombe 2,042 kwa
kuangalia mienendo yao
wakati wametumia pombe au
kutokutumia, walibaini kuwa kuna tofauti kubwa ya kimwili. Imebainika kuwa kunywa
glasi tatu kubwa za mvinyo
kunaweza kuusukuma mwili
kwenye kilele ambacho ni cha
kutumia zaidi chakula ndani ya
saa 24, ambacho kitampatia nguvu ya ziada, inaeleza
sehemu ya taarifa hiyo. Nguvu inayoongezeka kwa
kiwango hicho cha pombe
imebainika kuwa na 6,300 za
ziada tofauti na asingekunywa. Ikaonekana kuwa pombe
huchochea pia mtu kula
vyakula vyenye protini kwa
wingi hususan nyama. Pamoja na faida hiyo, ugunduzi
huo umebaini kuwa, watu
wanaokunywa pombe
wanajiingiza kwenye
mazingira mabaya ya
kuongeza uzito kupita kiasi. Kutokana na kula huko
kulikopitiliza, ugunduzi huo
umebaini wanywa pombe
wasipojitahidi kufanya
mazoezi wanajiweka katika
hatari ya kupata maradhi kama vile ya kisukari na moyo. Mtaalamu wa Lishe
aliyesimamia utafiti huo, Dk
Jacquie Lavin anasema
kinachoonekana ni kwamba
aliyekunywa pombe hopoteza
ule uwezo binafsi wa kujisimamia juu ya kiwango
cha chakula anachopaswa
kukitumia. Anasema wanaokunywa
pombe wana kawaida ya
kuongeza uwezo wa kula na
wanaweza kudumu mezani
kwa muda mrefu wakila, hasa
inapokuwa chakula ni kizuri na chenye lishe nyingi. Pombe hufanya chakula
kionekane bado kinahitajika
mwilini. Huwa inaamsha hisia
za kuona chakula ni kitamu
kuliko vile angekihisi katika
hali ya kawaida akiwa hajanywa pombe, anasema Dk
Lavin. Mtaalamu huyo wa Taasisi ya
Slimming World aliishauri
Serikali ya Uingereza iamuru
kampuni za vileo ziongeze
maelezo ya ziada kwenye lebo
zake. Miongoni mwa maelezo
aliyopendekeza ni vileo vyote
kuwa na maelezo kwamba
vinachochea uwezo wa kula
kwa kuwa huo ndiyo ukweli
kwa watumiaji.
MCL