GP
JF-Expert Member
- Feb 5, 2009
- 2,049
- 161
.....Inasaidia Kupunguza Magonjwa ya Moyo
Matokeo ya utafiti uliofanyika hivi karibuni kuhusiana na unywaji pombe umeonyesha kuwa wanaume wanaokunywa pombe kila siku wana uwezekano mdogo wa kupata matatizo ya moyo kulinganisha na wanaume wasiokunywa pombe kabisa. Utafiti uliofanyika nchini Hispania na kuwashirikisha wanaume 15,000 na wanawake 26,000 umeonyesha kuwa pombe inasaidia kupunguza theluthi moja magonjwa ya moyo kwa wanaume wanaokunywa pombe kila siku.
Hata hivyo pombe haikuonekana kuwa na faida yoyote kwa wanawake wanaokunywa kila siku.
Utafiti huo ulifanyika nchini Hispania ambako wakazi wake wengi ni walevi huku kukiwa na wagonjwa wachache wa matatizo ya moyo.
Utafiti huo ulihusisha wanawake na wanaume wenye umri kati ya miaka 29 na 69 ambao walitakiwa kuandika historia yao ya unywaji pombe na kisha kufuatiliwa afya zao kwa kipindi cha miaka 10.
Aina ya pombe walizokuwa wakinywa washiriki wa utafiti huo hazikuonyesha tofauti yoyote kati yao.
Jinsi pombe inavyosaidia kupunguza matatizo ya moyo bado haijakuwa wazi ingawa inajulikana kuwa pombe husaidia kuongeza kiwango cha lipoproteins mwilini ambacho huzuia kolestro zinazosababisha matatizo ya moyo kujijenga kwenye mishipa ya kusafirishia damu.
Hata hivyo wataalamu wameendelea kuonya kuwa unywaji wa pombe uliopita kiwango ni hatari na husababisha matatizo mengi ya kiafya ambayo husababisha vifo vya watu milioni 1.8 kila mwaka.
wapwa hii mnasemaje??
source