Pompeo afuta ziara yake barani Ulaya na Asia kushughulikia kadhia ya Iraq

Pompeo afuta ziara yake barani Ulaya na Asia kushughulikia kadhia ya Iraq

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo ameahirisha ziara yake nchini Ukraine na mataifa mengine barani Asia kufuatia shambulizi kwenye ubalozi wa Marekani mjini Baghdad lililofanywa na watu wenye silaha wanaoungwa mkono na Iran.

Pompeo alitarajiwa kuwasili Ukraine siku ya Ijumaa katika ziara ambayo ingemfikisha pia Belarus, Kazakhstan, Uzbekistan na Cyprus. Ofisi yake imesema Pompeo atalazimika kubakia mjini Washington kuendelea kufuatilia hali nchini Iraq ili kuhakikisha usalama na ulinzi wa raia wa Marekani kwenye kanda ya mashariki ya kati.

Siku ya Jumanne na Jumatano maelfu ya waandamanaji wanaoiunga mkono Iran waliuzingira ubalozi wa Marekani mjini Baghdad na kuchoma moto baadhi ya maeneo na wengine wakijaribu kuparamia kuta za jengo hilo.

Waandamanaji hao walikuwa wakipinga shambulizi la wiki iliyopita liliyofanywa na Marekani dhidi ya kundi la wanamgambo la Kataib Hezbollah.
 
Back
Top Bottom