Pongezi kwa CCM

Nyamodha

Member
Joined
Dec 7, 2022
Posts
6
Reaction score
1
CCM imemaliza Mkutano wake Mkuu wa 10 Kwa uchaguzi wa Viongozi wa Chama hicho ngazi ya Taifa.

Naipongeza CCM Kwa kuwa Chama bora Na chenye demokrasia ndani ya Chama sio tu katika Afrika, Bali pia hata ulimwenguni

Ni Chama kinachozidi kujijengea uimara, Na Kwa namna kinavyopendeka (sio tu Kwa wanachama bali wengi wa Watanzania), itavichukua vyama Vya upinzani miaka >100 kupata 'fursa' ya kuiongoza nchi hii.

Tukipe ushirikiano kituongoze kuelekea kwenye maisha bora.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi..
 
Mkutano huu umetufundisha ukifa tu unakuwa mbaya

Sasa kwakuwa sisi wote tutakufa basi hata aliesema siku akifa ety atakuwa mbaya

Hamna namna nyingine ya kuweka hii sentensi ila acha ibaki hivyo hivyo
 
CCM imemaliza Mkutano wake Mkuu wa 10 Kwa uchaguzi wa Viongozi wa Chama hicho ngazi ya Taifa.

Naipongeza CCM Kwa kuwa Chama bora Na chenye demokrasia ndani ya Chama sio tu katika Afrika...
Kwa miaka 60 hawajaweza kuleta maisha bora wataweza lini? Tuache usaliti kwa wananchi tafadhali!
 
Kwa miaka 60 hawajaweza kuleta maisha bora wataweza lini? Tuache usaliti kwa wananchi tafadhali!
Maisha bora Ni jitihada za pamoja za wananchi, CCM ikiwa mbele kama Chama kinachotawala.
Ndiyo maana kila Mtanzania Kwa nafasi Yake anapambana kupata maisha bora, huku CCM Na serikali Yake ikiwa imeweka Mazingira wezeshi kufanikisha azma hiyo: Maisha bora Kwa kila Mtanzabia.
 
Nyie "watiifu" kwa CCM ni watiifu zaidi kwa matumbo yenu kuliko kwa taifa letu. Mnashiriki kuwatesa na kuwaumiza watanzania kwa kutumia njia za kijanja lakini dhambi yenu ipo palepale.
 
Nyie "watiifu" kwa CCM ni watiifu zaidi kwa matumbo yenu kuliko kwa taifa letu. Mnashiriki kuwatesa na kuwaumiza watanzania kwa kutumia njia za kijanja lakini dhambi yenu ipo palepale.
Hata asiye mtiifu Kwa CCM ni mtiifu Kwa tumbo lake kwani tumbo ndo hukuwezesha kupumua!

Dhambi haiko CCM, dhambi ni ya MTU mmoja-mmoja, Na hii ndiyo sababu CCM itaendelea kutawala Kwa vile mnaodhani hamuitii CCM hamuitii hats jamii inayolindwa Na kulelewa na CCM (Watanzania) na hampendi kutambua jukumu zito la CCM kuyalinda na kuyasimamia maslahi ya Watanzania bila kujali wasioitii.

Amina!
 
Dhambi ya ulafi itapasua matumbo yenu nyie wajasiriatumbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…